Julia fox : sijafuata pesa wala umaarufu kwa kanye

Julia fox : sijafuata pesa wala umaarufu kwa kanye

Mambo yanazidi kunuoga huko Marekani, na leo katika mitandao ya kijamii kuna story ya mpenzi mpya wa Msanii Kanye West, Julia Fox ambaye amefunguka na kusema kuwa hajafuata pesa wala umaarufu kwa Kanye.

Taarifa hizo kutoka kwa Julia Fox amezitoa wakati akiwa kwenye Podcast na Forbidenn Fruits na kueleza kwamba, hajafuata pesa wala umaarufu kwa Kanye kwani maisha yake yote amekuwa kwenye mahusiano na mabilionea hivyo umaarufu sio hulka yake.

Mwanadada huyo amefunguka hayo baada ya walimwengu kumshambulia mtandaoni wakidai kwamba yupo kimapenzi na Kanye kwaajili ya ustaa na pesa na si kingine.

Na wewe msomaji wetu unaweza kudondosha comment zako katika ukurasa wetu wa Instagram ambao ni @mwananchiscoop.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post