John Cena atangaza kustaafu WWE

John Cena atangaza kustaafu WWE

Mwanamieleka wa Marekani John Cena ametangaza kustaafu kushiriki mashindano ya World Wrestling Entertainment (WWE) usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes Cena ametoa tangazo hilo liloleta mshangao kwa mashabiki wa mchezo huo kwenye sherehe WWE Money in the Bank nchini Canada.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 47, ambaye aliingia katika mieleke miaka 18 iliyopita, amedai kuwa shindano lake la mwisho katika mchezo huo litakuwa kama sehemu ya ziara ya kuaga mashabiki zake mwaka 2025 litakalofanyika Las Vegas nchini humo.

Cena mara nyingi anachukuliwa kuwa mmoja wa wanamieleka wa kitaalamu zaidi wa wakati wote na alipata hadhi ya bingwa wa dunia mara 16 tangu ajiunge na WWE mnamo 2001.

"Leo usiku natangaza rasmi kustaafu kwangu kutoka kwa WWE," aliwaambia mashabiki wa Toronto ambao walijibu kwa mshangao na baadaye kuimba "asante Cena". Alisema.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post