Jiongeze: Jentlomani wako hivi…

Jiongeze: Jentlomani wako hivi…

Kama hujaalikwa kwenye ishu, usiende mwanangu. ‘Samtaimzi’ hata ukialikwa usiende pia. Unaweza kualikwa na mtu ili useme hapana, kwa ushahidi tu.

Halafu tumechoka wewe kuwa kituko kila mara ukilewa. Kama pombe huziwezi acha, piga juisi au maji wakati sisi tunapiga monde. Siyo kesi, ni uwezo tu wa kuhimili tungi watu tunatofautiana.

Toa ‘tipu’ bila kuomba namba ya mhudumu, jifanye kama umetoa msaada tu. Hata simba siyo swala wote anawala huko porini, wengine anaacha na kupita zake.

Punguza kutumia simu sana, tena wakati mwingine kwa ishu ambazo hazina mpango. Wana wanaweza kukupuuza na kukunyima dili, ‘cozi’ unaleta ubwege.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags