Jiongeze: Ali Kamwe na ufalme wa Jangwani

Jiongeze: Ali Kamwe na ufalme wa Jangwani

Kwa sasa inajulikana yupi ni yupi pale Jangwani. Nenda kwenye kurasa zao mitandaoni, tazama ‘intaraksheni’ ya mashabiki wa timu yao. Kuna namna Kamwe anacheza na akili za mashabiki.

Mitaani mpaka mitandaoni anaishi kama sehemu yao. Anaweka picha kamili ya shabiki wa Yanga anayefanya kazi pale Yanga. Akiposti jambo la Yanga, hupata muamko mkubwa na hata lugha zake zinaenda na Wananchi.

Posti za wengine hazifungamani moja kwa moja na Wananchi. Wanashindwa kusoma alama za nyakati. Huu ni wakati wa kucheka zaidi ya kutafakari. Na hiki ndicho anachofanya Ally. Anachekesha kuliko kutafakarisha watu.

Jangwani kuna kila kitu. Makombe yote, wachezaji wakubwa, viongozi bora na mashabiki wa kweli. Unataka nini zaidi? Tafakari zaidi unapokuwa kwenye shida. Lakini furahia sana unapokuwa kwenye furaha.

Mbali na hilo, katika wasemaji waliopita Jangwani. Mpaka sasa Kamwe ana alama kubwa sana kwenye mioyo ya mashabiki. Na hii ni kutokana na ubunifu wake katika wakati ambao Yanga inaishi katika dunia yake.

Max Day, Master Key Day, Bacca Day, Pacome Day hizi ni alama za Kamwe. Kuna yale mabango baada ya kupeleka kipigo kwa watani wao. Ni ubunifu huu uliokwenda kujenga kuta za zege katika nyoyo za wananchi kwa Kamwe.

Ukifanya jambo kwa ajili ya watu utapata ufalme mioyoni mwao. Lakini ukifanya jambo kwa ajili yako. Yaani sifa binafsi, huwezi kupata hata Ukatibu Kata wa Kata ya Makata. Kamwe ni Mwananchi katikati ya Wananchi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post