Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za android

Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za android

Aisee!!! limekuwa jambo la karaha na wakati mwingine kufedhehesha pale unapoperuzi ukijaribu kutafuta hiki na kile mtandaoni au umefungua app fulani na ghafla tu unaona tangazo kuhusu kitu fulani mbele ya uso wa simu yako.

 Jambo hili linapoteza umakini wa kile ulichokuwa unakifanya kabla ya tangazo hilo kujitokeza, sometimes unachukia kabisa ila hakuna namna.

Hivi unafahamu sababu za matangazo hayo kujitokeza? Ngoja nikufahamishe hapa wasiofahamu basi mfahamu leo kwamba tangazo lolote linalojitokeza bila ya kutarajia au linabadilika badilika ni matangazo yaliyo chini ya Google (Google Ads) kwa mantinki ya kumuingizia kipato yule ambaye tangazo hilo limejitokeza kwenye tovuti yake.

Usiboreke, mbinu hizi hapa za kutumia ili kuzuia matangazo kwenye simu janja yako.

Tumia kivinjari cha Opera Mini

 Moja ya sifa kuu kuhusu kivinjari cha Opera Mini ni kuwa na uwezo wa kuzuia matangazo yanayojitokeza tu, uwezo huo upo ndani kwa ndani ya kivinjari cha Opera Mini.

Tumia Ad-Block Browser

Hiki ni kivinjari kinachopatikana kwenye soko la programu tumishi kwa wanatumia Android hivyo kinaweza kuwa mbadala wa kivinjari kwa dhumuni kuu la kuondokana na kadhia ya matangazo yasiyokuwa na mpangilio wowote.

Mpangilio (settings) kwenye kivinjari cha Google Chrome

Kupitia kivinjari cha Chrome pia inawezekana kabisa ukazuia matangazo ambayo yanatokea tu bila yeye kufahamu, Kitu cha kufanya ni kuingia kwenye Settings>>Site settings>>Pop-ups, kisha unachagua Blocked.

Tumia Data Saver Mode kwenye kivinjari cha Chrome

Kinjari cha Chrome kina njia ya pili ya kuweza kupambana na matangazo yanayotokea tu bila ufahamu pale mtu anapoperuzi, Pia kwa kufanya kipengele cha Data Saver kuwa wazi (on) basi utapunguza utumiaji mkubwa wa kifurushi cha intaneti na kufanya kivinjari kuperuzi kwa kasi na kumfanya mtu akifurahie.

Ayeyeeee bila shaka tutakua tumefahamiana hapoo, enjoy your smartphone mambo ni motooooo!!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post