Jinsi ya kuwajibika kazini

Jinsi ya kuwajibika kazini

I hope mko good wafuatiliaji wa segment ya kazi, sasa leo niko na kitu serious kidogo, kama tunavyojua kila mtu anatafuta kazi ili afanye hiyo kazi na aweze kupata anachokistahiri lakini sio wewe unapata kazi kisha unaichezea mdako kuna wenzio wanaitafuta my wangu siku ikija kuondoka hiyo kazi utasaga meno kwa kulia.

Kwanza kabisa unapopata kazi lazima ufanye kazi kweli na uwajibike haswa maana awaajiri watakapoona mwenendo wako wa kazi si mzuri hawatakuwa na urafiki na wewe tena. So hapa leo tutaelekezana kuhusiana na namna au jinsi ya kuwajibika ukiwa kazini.

Kuwajibika kazini kunamaanisha kuwa unafanya bidii kufanya kile ulichosema utafanya na kwamba upatiwe adhabu usipoifanya. Ikiwa uko tayari kuifanyia kazi, unaweza kuchukua hatua fulani ili kufanya vyema zaidi katika nia yako ya uwajibikaji.

      Jiwekee malengo ya binafsi, madogo na makubwa.

Malengo madogo yanaweza kuwa mambo kama vile kusoma barua pepe zako zote au kufanya kila kitu kutoka kwa orodha yako ya kazi kabla ya kuondoka siku hiyo.

Malengo makubwa yanaweza kujumuisha kuvuka lengo lako la mauzo kwa mwaka. Unapofikia malengo yako, unaweza ukajipongeza hata kwa zawadi inayakustaili. Pia usisahau kupanga likizo zako.

 

      Fuata kile unachosema utafanya.

Ikiwa utaweka tarehe ya mwisho na mteja au kuahidi kumaliza mradi kwa tarehe fulani, hakikisha kuwa unaweza kuufanya. Usipotimiza kazi zako kwa wakati jambo hilo linaweza kupelekea sifa yako kuharibika usipotimiza ahadi yako.

Ili kutimiza ahadi zako, huenda ukalazimika kuwauliza wengine kupata mahususi kuhusu tarehe, nyakati au maelezo ya kile wanachotarajia kutoka kwako, ili ujue ni jinsi gani na lini unahitaji kukamilisha mradi au kazi uliyoahidiwa.

      Kubali matokeo either yawe hasi au chanya

Iwapo umefanya uwezavyo katika kazi yoyote iliyopo na bado ukashindwa, usifadhaike au kulaumu hali hiyo kwa mtu au kitu kingine. ila wajibika, na ukubaliane na matokeo.

      Jitahidi ujue madhaifu yako

Unaweza kuonekana kama kichaa kuuliza kwa undani juu ya mambo unayofanya vibaya, lakini ni njia moja wapo ya kumfanya boss wako aeleze kile unachohitaji kufanya ili kupata mafanikio kwenye kazi.

Ukifanikiwa kumfanya boss wako afanye mapitio, usimwachie boss wako kueleza kila kitu kwa kina na rudi ofisini kwako ukiwa na maswali mahususi kuhusu utendakazi wako na jinsi unavyoweza kuuboresha.

Kingine cha kuzingatia ni kutokupelekesha hapa namaanisha wajibu wako unaujua siyo kila saa boss wako akwambie fanya hichi fanya kile jifunze kujituma na kujisimamia mwenyewe.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post