Jinsi ya kutengeneza Simple Dessert

Jinsi ya kutengeneza Simple Dessert

Katika sehemu za kuuzia vyakula mbalimbali nchini, watu wameonekana kuvutiwa na kinywaji cha dessert ambacho huwa kina mchanganyiko wa matunda na maziwa na yogurt.

Hivyo basi na mimi leo sina budi kukusogezea kinywaji hicho bwana, watoto wa mjini wanakwambia soda waachie wazee, siku hizi ni mwendo wa dessert drink na katika kinywaji hichi kuna aina mbalimbali kama ilivyo kwenye soda na kuna hadi dessert za cake.

Kinywaji hichi unaweza kunywa na chipsi, burger, pizza na hata biriani ni wewe tu utapenda kula na kitu gani, bei yake inaanza na shilingi elfu tatu nk. hivyo basi ukipata sehemu nzuri ya kuuza kinywaji hichi utakuwa umetoboa sana mtu wangu wa nguvu.

Haya ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua dondoo za utengenezwaji wa kinywaji hicho, na leo nimekusogezea dessert ya mchanganyiko wa matunda mbalimbali.

Mahitaji

  • Ndizi
  • Zabibu
  • Pears (liliova laini)
  • Nanasi
  • Strawberry
  • Embe

Yogurt na hapa wengine hutumia maziwa ya kawaida siyo lazima uwe na yougurt

Asali

Cinnamon powder kidogo sana (1/4 kijiko cha chai)

Matayarisho na jinsi ya kuandaa

  • Safisha matunda yote kisha yakaushe maji baada ya hapo yakate vipande vidogo vigogo kisha yatie kwenye bakuli safi.

Baada ya hapo weka cinnamon na yogurt vichanganye vizuri kisha chukua vipande vyako vya fruits changanya katika mchanganyiko wako na wakati wa kuandaa utatanguliza asali kidogo ndiyo uweke dessert yako.

Na mpaka hapo itakuwa tayari kwa matumizi, unaweza kunywa hapo hapo au ukaweka kwenye friji ili kupata baridi kidogo.

NOTE: Dessert ni kinywaji ambacho ni kizuri kwa afya ya mlaji kwa sababu haina sukari pia ina mchanganyiko wa matunda hivyo basi ni vizuri zaidi kukitumia kuliko soda.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags