Jinsi ya kutengeneza sabuni za maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni za maji

Ni matumaini yangu mko pouwa kabisa, leo kwenye biashara nimekuja na wazo konki ambalo halitakufanya ulale njaa, kutokana na watu kila siku kutumia sabuni katika matuminzi yao mbalimbali.

Kwa siku za hivi karibuni sabuni za maji zimekuwa zikitumika kwa wingi kutokana na kutokuwa na gharama kubwa, pia zipo zinazoweza kutimiwa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kufulia nguo, kuoshea nywele na hata kudekia choo.

Sehemu ambayo biashara hii inafanya vizuri zaidi ni katika nyumba za kulala wageni ambapo hutumika kufanyia usafi, mara nyingi bei yake huanzia elfu 10 kwa lita moja.
Mahitaji
 Sulphonic Acid lita 1
 Soda Ash robo kilo
 Sless au Ungalol lita 1
 Glyceline vijiko vitano vya chakula
 Rangi kijiko kimoja
 Chumvi gram 750
 Tigma ya 3000
 Pafyum laini ya matunda au ya harufu uitakayo.
 CDE mls 2000
 Maji safi lita 40
Baada ya kupata vifaa hivyo fuata hatua hizi.

Chukua maji lita 40 gawa mara mbili ili upate lita 20, kisha lita 20 moja tia Tigna yote koroga hadi upate uji mzito kisha weka kando, weka Sulphonic acid kwenye chombo kisha tia Soda koroga vizuri hadi upate kitu kama ugali, hakikisha unakoroga vyema kwa muda wa dakika 20 bila kupumzika.

Ongeza Sless koroga vizuri kwa dakika 10 weka maji lita 20 ambayo hayana Tigna kisha koroga hadi donge lililo kama ugali liishe lote (tumia fagio la chelewa safi kukorogea ili kurahisisha kazi, au mwiko mkubwa kabisa wanaotumia kupikia kwenye sherehe).

Baada ya zoezi hilo weka yale maji yenye Tigna koroga vyema kisha ongeza rangi na glyceline CDE endelea kukoroga hadi iishe mwisho weka pafyum na ukoroge kwa dakika 5.

Ifunike na uiache kwa saa 24 na zaidi ndiyo uweke kwenye vifungashie kama vile kwenye madumu, au chupa kazi ni kwako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags