Jinsi ya kutengeneza peanut butter

Jinsi ya kutengeneza peanut butter

Haya kumekucha jamani siku zinakimbia hatuna muda wa kujieleza, mwendo ni uleule kufanya biashara na kuongeza kipato si kukaa kizembezembe.

Leo katika segment yetu ya biashara tumekusogezea kitu konki namna ya kutengeneza peanut butter au siagi ya karanga ukiwa nyumbani kwa njia rahisi kabisa.

Kama tunavyojua kwa miaka ya hivi karibuni familia nyingi huwa zinapendelea kutumia siagi ya karanga katika matumizi mbalimbali mfano kula na mkate kuweka kwenye mboga nk. Kuliko hapo awali watu walizoea kutumia blueband tuu.

Sasa ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujua mahitaji ya kutengeneza butter hiyo na jinsi ya kutengeneza, ukumbusho tuu ukishasoma ukaelewa basi inabidi ujaribu mara kwa mara mpaka uweze kabisa ndio utengeneze kwa ajili ya biashara.

 

MAHITAJI

      Karanga vikombe 2

      Asali au sukari kijiko kimoja na nusu cha chakula

      Mafuta ya kupikia kijiko kimoja na nusu cha chakula

      Chumvi 1⁄2 kijiko cha chai

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA/KUTENGENEZA

      Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe, hapa sasa unaweza kuzikaanga na mchanga kama wanavyokaanga wale waonauza ili kuepukana na kuziunguza.

      Kisha ziache zipoe kabisa na uanze kutoa maganda yote usiache ganda hata moja, ukiacha maganda utasababisha butter yako kuja kuwa chungu badaaye.

 

      Mimina karanga, chumvi na mafuta katika food processor au blender , saga hadi iwe laini

      Ongeza asali, chumvi, sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini kabisa, ukiwa unasaga utaona tuu itaanza kubadilika yenyewe.

      Na mpaka kufikia hapo utaitoa katika chombo ulichosagia na kuweka katika contena uliyotayarisha kwa ajili ya kuwekea weka nenda kaihifadhi kwenye friji ikipoa itakuwa tayari kwa matuminzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags