Jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi kwa ajili ya biashara

Hakikisha haukai kizembe ndugu yangu changamsha akili na maarifa au siyo? Leo nakupa hii hapa jinsi ya kutengeneza mafuta ya Nazi simple kabisa bila mambo mengi.

Kama tunavyojua siku hizi watu wengi wanapenda kupaka mafuta na ni bidhaa ambayo hutokana na Nazi yenyewe ambayo hufanya kazi nyingi sana mwilini ikiwemo kuondoa makovu, mabaka na kuacha mwili ukiwa laini, safi na wenye kunawiri haswaaa.



MAHITAJI .
1, Nazi yako iwe safi na nzima sio mbovu
Andaa sufuria yako kwa ajili ya kupikia mafuta jikoni, hakikisha una ‘blenda’ au kibao cha mbuzi kwa ajili ya kukunia nazi ili uweze kupata tuwi la nazi.

2, Uwe na Chujio kwa ajili ya kuchuja machicha ya nazi na kuweza kupata tuwi haliyakuwa safi kabisa. Andaa jiko lenye moto ambalo litatumika kwa ajili ya kuchemsha mafuta ili yaweze kujitenga na maji.

JINSI YA KUTENGENEZA
Kwanza andaa nazi zako zikiwa safi hasaa
Kisha kuna nazi zako kwa kutumia kibao cha mbuzi au kama una ‘blenda’ unaweza ukatumia kupata nazi iliyokunwa.

Ukishapata nazi iliyokunwa unatakiwa kuichuja kwa kutumia chujio ili kupata tuwi la nazi na unaweza ukaongeza maji kidogo ili kupata tuwi jingi kidogo na hilo tuwi ndio ambalo tunalolihitaji kwa ajili ya kulitumia.

Kisha utailaza tuwi lako mpaka kesho ili kutenganisha maji na tuwi na mafuta hapo litatengeneza tabaka, kisha utatoboa hilo tabaka ili kutoa maji yote ndani ya tuwi lako.

Kisha sasa bandika jikoni ilo tuwi lililoganda ili kupata mafuta halisi halafu baada ya kubandikwa katika moto yatabadilika na kuwa safi kabisa bila tatizo lolote.

Na hapo yatakuwa tayari kwa kutumia yaani hapa hatuongezi kemikali ni mwendo wa natural tuu!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags