Jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi

Jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi

Biashara ya mafuta asili inazidi kukua kwa kasi kila uchwao, watu mbalimbali wamechukulia bidhaa hiyo kama sehemu ya kujipatia kipato.
Mafuta ya nazi ni bidhaa ambayo hutokana na nazi yenyewe ambayo hufanya kazi nyingi mwilini ikiwemo kuondoa makovu, mabaka na kuacha mwili ukiwa laini, safi na wenye kunawiri haswaaa.

Kutokana na biashara hii kufanya vizuri sokoni tumeona tuwaletee namna ya kutengeneza mafuta ya nazi kwa ajili ya biashara.
Mahitaji yake.
• Sufuria nzito ambayo haishiki chini kwa haraka (haiunguzi)
• Nazi nzima siyo mbovu kuanzia 10-15
• Kibao cha mbuzi au blenda kwa ajili ya kukuna nazi
• Chujio
• Maji
Jinsi ya kutengeneza
Safisha nazi zako kwa maji kisha anza kuzikuna au kuzisaga mpaka ziwe laini, katika kukuna unabidi uwe muangalifu ili usitoe mapande makubwa, nazi iliyokunwa inatakiwa iwe laini nimerudia kwa sababu ya msisitizo.

Ukipata nazi iliyokunwa unatakiwa kuichuja kwa kutumia chujio ili kupata tui , sasa hapa ndiyo unaweza kuchanganya na maji kidogo ili kupata tui, hilo tui ndiyo tunalihitaji kwa ajili ya kutengeneza mafuta.

Ukimaliza kuchuja utaliweka kwenye chombo kisafi kikubwa na utaliacha mpaka kesho ndiyo uendelee na process nyingine, tui hilo likishalala litajitengenisha maji yatayojitenga na tui, unachotakiwa kufanya ni kutoa maji na kuacha tui lenyewe.

Ukimaliza kuchuja bandika jikoni tui lako na kuliacha lichemke mpaka lichuje mafuta halisi, ukipata mafuta yako yaache yapoe na uanze kupaki kwenye chupa zako.

Mafuta haya ni mazuri kwa ajili ya kupaka, kwenye nywele, mwilini pamoja na kupaka watoto wachanga ambao huzaliwa ngozi ikiwa na vipele, bei yake huanzia elfu tatu kwa chupa moja, changamkia fursa hiyo acha kukaa kizembe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post