Jinsi ya kutengeneza kashata za karanga kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kutengeneza kashata za karanga kwa ajili ya biashara

Hellow! Vipenzi vyangu kama kawaida yetu ni mwendo wa biashara tuu, vipi kwanza edi iliendaje pande hizo, basi mkala nyama zenu bila kunialika, ila hakuna shida tuendelee na kilinacho tukutanisha kila siku.

Leo katika biashara tumekuja na pishi jingine ambalo pichi hili tunapika kwa ajili ya biashara tuu, sasa leo nimekuja na kitu ambacho sio watoto tuu wanapenda hadi watu wazima wanakikubali sana.

Kashata za karanga inajulikana kuwa zinaliwa na watu wazima wakiwa katika mikutano yao ya kunywa kawaha lakini sasa hivi hadi wanafunzi wa shule za mzingi wanazielewa mno, juzi kati nilipita shule moja nikakutana na mwanamama anauza kashata nje ya shule, jamani jamani kusema za ukweli sikutegemea, basi nikaona isiwe tabu bora tujuzane ili wote tupate pesa.

MAHITAJI

  • Karanga - Kilo moja
  • Sukari - nusu na robo
  • Maji - 2 vikombe
  • Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai (UKIPENDA)

 

NAMNA YA KUTENGENEZA
Step 1:  Chagua karanga zako vizuri na utoe zile zote zilizo oza kwani hufanya kashata zako kuwa za Uchungu, Pia toa karanga zote zenye kuonyesha ukungu maana kitaalamu hiyo ndiyo sumu hivyo usipotoa huwa na madhara kwa walaji wako.

Step 2: Baada ya hapo kaanga karanga zako mpaka ziive vizuri lakini pia uwe makini kuangalia karanga zako zisiungue maana zikiungua kashata zako zitakuwa na uchungu wakati wa kula na zitakuwa na harufu mbaya.

Step 3: Zikisha iva epua na uziache zipoe na karanga mina tabia ya kuivia chini hivyo uwe makini wakati wa kukaanga unaweza ona zimekauka lakini baada ya kumimina kwenye ungo zinapo poa zinaendelea kujikaanga kutokana na ule moto uliokaangia

Step 4: Ukimaliza toa maganda yote kisha zichague tena vizuri na ukimaliza saga karanga zako mpaka zilainike kiasi au Kama utapenda laini Sana pia ni sawa, unaweza endelea kusaga mpaka utakaporidhika mwenyewe kulingana na soko lako kwa maana ya wateja wanataka kashata za aina gani.

Step 5: Kisha changanya maji na sukari kwa uwiano, weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira.

Step 6: Changanya unga wa karanga (Karanga hakikisha zimesagwa/kutwangwa) na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.

Step 7: Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata

Step 8: Paka mafuta treyi lako kisha mimina na utandaze upesi upesi

Step 9: Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha kashata zako zipoe kabisa harafu panga kwenye sahani au bakuli tayari kwa kwenda sokoni.

 

Naaam! Kama kawaida yetu kauli mbiu ni ile ile usikurupuke tuu ukasema leo naamka natengeneza kashata kwa ajili ya biashara bali unatakiwa kufanya mazoezi hata mara mbili au mara tatu kwa kujifunza ili uwe ukija kuzitengeza uwe mtaalamu Zaidi.

Oky oky I hope kila siku tunaenda sawa watu wangu wa nguvu yaani mwendo ni uleule hakuna cha kututengeniasha na biashara so niwewe tu kuamua kuchakarika ili uweze kujipatia pesa yako ya halali, wanasemaga pesa ya jasho lako ni tamu kuliko ya kuomba.

 






Comments 1


  • Awesome Image

    Hbr naomba kujua namna ya kupika karanga nzimanzima ambazo hazijakaangwa zile za kuweka unga ngano

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags