Jinsi ya kutengeneza karanga za mayai kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kutengeneza karanga za mayai kwa ajili ya biashara

Oyaaaweeeeh! Kwahiyo tumekubaliana kuwa hakuna cha kututenganisha na kufanya biashara, yaani sasahivi nimekuja na moto wa kuotea mbali, kama kawaida yangu sinaga mba mba mba katika kuwaeleza swala zima la kuchakarika ili tuweze kupata pesa.

Mpaka hapa tulipo fikia yaani staki kuskia mtu anakaa kizembe zembe kisa hana kibiashara cha kufanya, utakuwa unatania wewe, maana safari hii nimekuja kivingine kabisa nawaletea vyuma tuu.

Sasa leo bwana katika segment yetu ya biashara na ujasiliamali nakusogezea kabishara kadogo lakini kanafaida sana, so ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua jinsi ya kutengeneza, ili nawewe usibweteke upate cha kufanya.

MAHITAJI

  • 2 vikombe vya karanga
  • 1½ vikombe vya unga wa ngano
  • ½ kijiko cha chai cha baking powder
  • ¾ kikombe cha sukari
  • 1½ kijiko cha chakula cha pilipili ya unga
  • 1½ kijiko cha chai cha pilipili manga ya unga
  • ¾ kijiko cha chai cha kungumanga
  • 1 kijiko cha chai cha chumvi
  • 2 mayai
  • Mafuta ya kupikia kwa ajili ya kukaanga

MAELEKEZO

Step 1: Jaza maji ya kutosha kwenye sufuria ya ukubwa wa wastani, kwa ajili ya kuchemsha karanga. Weka sufuria lenye maji kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha maji yachemke. Maji yakianza kuchemka, weka karanga, kisha funika na acha zichemke kwa muda wa dakika 3 hadi 5.

Step 2: Epua karanga na uzime jiko, Chuja maji yaliyomo kwenye karanga kwa kutumia chujio, ili ubakiwe na karanga peke yake. Mimina karanga kwenye sinia, kisha zisambaze ili zikauke maji.

Step 3: Changanya pamoja kwenye bakuli kubwa unga wa ngano, sukari, pilipili ya unga, pilipili manga ya unga, baking powder, kungumanga na chumvi.

Step 4: Chukua mayai, yavunje kisha umimine ute pamoja na kiini chake kwenye bakuli ndogo. Yapige mayai hayo, kisha yamimine kwenye sinia lenye karanga. Chukua bakuli lenye mchanyiko wa unga wa ngano pamoja viungo vingine, na umimine kwenye sinia nusu ya unga huo, kisha changanya vizuri kwa kutumia mikono yako.

Step 6: Zisambaze kwenye sinia karanga ulizokwisha zichanganya, huku ukitenganisha karanga zilizoshikana. Nyunyizia juu ya karanga nusu iliyobakia ya unga wa ngano wenye viungo mchanganyiko, kisha acha kwa muda wa dakika 8 hadi 10.

Step 7: Weka kikaango chako kwenye jiko lenye moto wa wastani. Weka mafuta ya kupikia ya kutosha kisha acha yapate moto. Mafuta yakishapata moto, weka karanga kiasi kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara hadi utakapoona karanga zako zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

Step 8: Toa karanga zilozoiva na uziweke kwenye bakuli lenye karatasi za taulo (paper towel), ili zipoe na kujichuja mafuta. Endelea kukaanga karanga nyingine zilizobakia, hadi zote zitakapoisha.

Ukishamaliza unasubiri karanga zako zipoe na sasa tayari kwa kula au kufunga katika package kwa ajili ya biashara.

Kama ilivyo kawaida yetu, kama hujawahi kutengeneza hata siku moja basi inabidi ujaribu hata mara 3 au mbili ili siku ukija kutengeneza kwa ajili ya biashara basi hakuna kitakacho kuwa kigumu kwa upande wako. Sina Zaidi ya kusema tukutane tena wiki ijayo katika somo linguine byeee!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags