Jinsi ya kurudisha picha na video kwenye simu yako

Jinsi ya kurudisha picha na video kwenye simu yako

Yees! Mambo vipi mdau wa kipengele cha smartphone kama kawaida kila jumatano huwa tunajifunza mambo mbalimbali yanayohusu simu zetu.

Leo bwana nimekuandalia dondoo inayohusu jinsi ya kurudisha picha au video ambazo umezifuta kwenye simu yako aidha kwa bahati mbaya au ulidhamira na hujui namna gani zitarudi twende sawa mtu wangu ujanja ni huu hapa.

Ebwana jambo la  kufuta picha au video  ni kitu ambacho kimezoeleka na huwenda mtu anakuwa amefuta kwa bahati mbaya au akiwa amekusudia kuzifua, Imethibitika kuwa inawezekana kurudisha picha au video ambazo zimefutwa kwenye simu janja yako.

Aisee kuweza kurudisha vitu vilivyofutwa kwenye simu janja si jambo rahisi lakini pia linahitaji umakini mkubwa wakati wa kufanya jitihada kuweza kurudisha data zako kwenye simu.

Hatua za kufuta wakati wa kurudisha vitu vilivyofutwa kwenye simu janja yako hizi hapa.

  • Pakua Android Data Recovery. App hii ndio itakayokuwezesha kurudisha picha/video ambazo zilikuwa zimefutwa, Baada ya kuipakua app hii unganisha simu yako kwenye kompyuta kwa kutumia USB.
  • Ruhusu USB debugging’, Hatua hii ya pili itawezesha simu yako iweze kufanya kile ambacho unakikusudia kwa msaada wa app hii, Ingia Settings>>Developer Options>>USB debugging. Bofya ok baada ya USB debugging kufunguka.

Anza kuchagua mafaili ya kurudisha. Baada ya simu yako kutambuliwa kwenye kompyuta, programu hii maalum itakuleta kwenye ukurasa ambao utakuruhusu kuchaguadata unazotaka kurudisha.

Bofya “Scan” ili ziweze kusafishwa baada ya kumaliza kuchagua data unazozitaka zirudi. 

Baada ya data kuwa zimeshasafishwa; kwanye simu janja yako kitatokea kiboksi ambacho utakakiwa kubonyeza “Allow” na kama hakitatokea basi bofya “Retry“. 

  • Kurudisha data. Hii itakuwa ndio hatua ya mwisho, Baada ya mchakato mzima wa kusafisha data zilizofutwa (picha, video, sms, n.k) itakubidi uchague vile unavyotaka kurudisha na baada ya hapo utabofya “Recover“.

Note: Ni muhimu kuzingatia kwamba simu yako inakuwa na chaji zaidi ya 20% ili kuepuka kuzimika kwa simu jambo linaweza kusabisha matatizp kwenye simu janja yako.

Nikukumbushe tu kuwa makini sana pale unapotumia simu ili kuepuka kufuta vitu muhimu kwenye simu yako .

 Ebwana eeeh!! This is smartphone bila shaka itakua tumefahamiana vizuri kabisa mtu wangu kama kunanjia nyingine ambazo unazifahamu basi unaweza ukajiongeza pia nakutakia siku njemaaaaaaaaaa!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags