Jinsi ya kupika vitumbua vya biashara

Jinsi Ya Kupika Vitumbua Vya Biashara

Mambo vipi? karibu kwenye ukurasa wa nipe dili,kama kawaida huwa tunapeana madili mbalimbali kuhakikisha kwa namna moja au nyingine unapata fursa ya kujiingizia kipato.

Leo kwenye kipengele hiki utakwenda kujifunza jinsi ya kupika vitumbua vya biashara, yes twende sawa ili uweze kunufaika katika hili, karibu.

 

Hakikisha unazingatia maelekezo ili kazi yangu isiwe ngumu na uweze kutoa vitafunwa vizuri.

 
Vipimo

1 Kikombe cha mchele.

1 Kijiko cha kulia cha unga wa ngano.

3/4-1 Kikombe cha tui la nazi zito.

2 Mayai.

1 Kijiko cha chai cha hamira.

1/2- 3/4 kikombe cha sukari.
Hiliki kiasi upendacho.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

Hakikisha una osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja.

Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.

Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.

Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike,Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.

Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.

Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.

Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia. Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.

Yes hapo sasa unaweza kupanga  kwenye sahani, kwani vitumbua vyako tayari na unaweza kula vikiwa vya moto au vikipowa enjoy mapishi mtandaoni!!!

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post