Jinsi ya kupika visheti kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika visheti kwa ajili ya biashara

Alooooooooo! Msishangae sana ndugu zangu ndo maisha, kila siku sio lazima tuzungumzie kuhusiana na mada furani, leo tunaibuka kivingine katika segment yetu ya biashara.

Kuna wanawake wengi mtaani wanalalamika kuhusiana na ajira watapata wapi, wanajitahidi kutafuta lakini hawapati nachotaka kuwaambia tuu chochote unacho kidharau ndicho hicho ambacho watu wengi kimeweza kuwatoa kimaisha. 

Watu wengi wamekuwa waki dharau baazi ya biashara ndogo ndogo za watu lakini bila kujua tuu ndio hizo hizo zinazo watoa kimaisha, leo nikaona hapana wacha nije na pishi ambalo halitaki gharama sana ila ukiweza kupata wateja kama wanafunzi linaweza kukutoa kimaisha niamini mimi.

Wadau wa jikoni, leo na ambao wako radhi kufanya biashara tuna visheti (vikokoto), ni aina ya kitafunwa ambacho kinaweza kuliwa na kahawa, chai, juisi na hata maji. 

Ila kwa chai na kahawa vinapendeza Zaidi, Kuna namna tofauti tofauti za uandaaji wa visheti, kwasababu kuna wengine hukandia nazi, mara nyengine mafuta, siagi na hata maziwa. Vya leo tutatumia siagi, na tukijaaliwa siku nyengine tutapika na hizo aina nyengine. 

MAHITAJI

  • Ngano kilo1
  • mafuta lita1
  • siagi robo kilo
  • yai 1
  • Hiliki kiasi
  • baking powder kijiko1
  • Chumvi kidogo sana
  • Sukari nusu

MAELEKEZO

  1. Chunga unga wako, weka baking powder, tia chumvi kidogo ukipenda, tia sukari kidogo na hiliki changanya na siagi uvuruge
  2. tia mafuta nusu kikombe, endelea kuvuruga unga wako
  3. piga yai litie kwenye unga, endelea kuvuruga
  4. ongeza maji kiasi ili unga wetu uweze kukandika na kushikana kuwa donge moja
  5. Tengeneza vidonge vidonge, kisha uviviringishe hadi viwe kama fimbo, baadae weka kwenye kibao ukatekate visheti vidogodogo
  6. Weka mafuta kwenye karai jikoni, yakipata moto kaanga visheti hadi viive, kisha vitoe pembeni uanze kuandaa SHIRA
  7. Andaa shira kwa kutumia sukari nusu, na maji kikombe cha chupa ya chai kimoja, bandika jikoni maji ulotia sukari yachemke hadi yatoe povu na ukiitoa kidogo ukiishika inanata sana, hapo shira itakuwa tayari.
  8. Visheti ulokaanga weka kwenye sufuria ya shira, weka na hiliki, kisha vipetepete ili vijigeuze na kuenea sukari vyote. Vikiwa tayari vimekaukia sukari vizuri, visheti vyetu weka kwenye chombo tayari kumfikia mlaji.

Visheti vyetu tayari wadau, mimi hupenda hivi vya kukandia siagi sababu hukaa muda mrefu bila kuwa vigumu. Kwa hiyo waweza tengeneza ukala na vikibaki unavihifadhi vizuri kwa ajili ya kutafuna siku nyengine.

Kama unavyojua lengo letu sio kula, ni kufanya biashara unachotakiwa kufanya ni kutafuta package za size tofauti tofauti na uanze kujaza, na hivi wateja wake wengi ni wanafunzi unaweza kuomba shule ilio karibu na wewe n ahata maduka ya mangi pia I hope utapata wateja ukitengeneza kitu kizuri.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags