Jinsi ya kupika tambi za dengu kwa ajiri ya biashara

Jinsi ya kupika tambi za dengu kwa ajiri ya biashara

Hellow vipenzi vyangu kama mnavyojua kuwa maendeleo hayana chama basi nami sina hiyana kuwaelekeza yale yote yanayohusiana na ujasiriamali na kuchakalika, mwendo ni ule ule hatupoi wala hatuboi mpaka kieleweke.

Uzuri kazi nyingi za siku hizi hazihitaji uwe mwananke au mwanaume kama hapo awali ilivyozoeleka siku hizi kazi kazi ndio maana tunaendelea kuelimishana kuhusu biashara mbali mbali, na leo nimekuja kukujuza au kujuzana kuhusiana na jinsi ya kutengeneza tambi.

Tambi ni snacks ambazo watu wengi hupendelea kunywa na juice pindi wawapo safarini au hata nyumbani. Ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujua mahitaji na jinsi ya kuzitengeneza.

MAHITAJI

  1. Unga wa dengu 1⁄2 kilo
  2. Binzari nyembamba 1⁄2 kijiko cha mezani
  3. Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
  4. Unga wa mchele 1⁄4 kilo
  5. Chumvi kiasi
  6. Mafuta ya kula 1⁄2 lita
  7. Baking powder

JINSI YA KUPIKA

1.Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu kisha nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga.

2.Baada ya hapo changaya vizuri na kisha weka maji kidogokidogo huku ukiukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.

3.Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa.

4.Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.

5.Weka kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Epua na weka pembeni, weka kwenye sahani safi na kavu  mpaka kufikia hapo tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Uzuri wa pishi hili bwana haina kurudia ili ujue kupika bali ukishajua kupangilia vipimo na mahitaji yako vizuri basi, na kitu cha msingi ni kuwa snacks hizi zinauzika sana mashuleni na sehemu za madaladala changamkia furasa hiyo mwanangu sana unakaaje kizembe.

Nasemaje nasemaje kaa mkao wa kula next week nina jambo langu!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags