Jinsi ya kupika skonzi kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika skonzi kwa ajili ya biashara

Leo katika biashara mwendo ni ule ule tunapeana madini kuhusiana na kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya biashara na leo tunajuzana na kufundishana  jinsi ya kuandaa skonzi.

Skonzi ni mkate unaopendwa na wengi pia ni rahisi kutengeneza. unaweza kuliwa kama kitafunwa cha chai asubuhi, au mlo kamili wa mchana na jioni ukisindikizwa na supu au mchuzi.

Kitu cha kuzingatia katika kutengeneza mkate, vipimo ni muhimu sana katika kuoka, kama unataka matokeo mazuri katika uokaji, fuatilia vipimo kama vilivyo, kamwe usikadirie chochote.

 

Tumia vikombe na vijiko maalum kwa kupimia ili kupata matokea mazuri zaidi.

MAHITAJI

1              Pakti 1 ya hamira

2              1/4 kikombe maji ya uvuguvugu

3              Vijiko 2 vya chakula sukari

4              Vikombe 2 unga wa ngano

5              1/2 kijiko cha chai chumvi

6              1/2 kikombe maziwa

7              Vijiko 2 vya chakula siagi; na ya ziada ya kupaka juu

Ukiwa unapendelea mkate wako uwe mtamu zaidi unaweza ukaongeza maziwa pamoja na siagi ila kama hauna basi unaweza kuaendelea na ulivyoandaa.

JINSI YA KUTENGENEZA

Changanya maji ya uvuguvugu, hamira, chumvi na sukari kwenye bakuli kubwa kisha funika na kitambaa acha mchanganyiko uumuke kwa dakika kama 5.

Ukiumuka ongeza maziwa, kikombe 1 cha unga wa ngano pamoja na vijiko 2 vya chakula vya siagi iliyolainika au kuyeyuka, Kisha kanda taratibu.

Ongeza kikombe kingine cha unga wa ngano kidogokidogo huku unakanda mpaka unga ushikane.

Kama unga utakuwa unanata sana, ongeza unga wa ziada kidogo kidogo mpaka ushikane kabisa, Usikande kwa muda mrefu, ukikanda sana skonzi zitakuwa siyo laini sana

Ukimaliza kukanda, funika tena bakuli na kitambaa kwa dakika kama 30.

Paka mafuta chombo cha kuokea. Kanda unga tena kisha ugawanye kwenye madonge 9 mpaka 12. Mimi ninapenda kubwa kwa hiyo niliweka mara 9. Funika tena na kitambaa, acha unga uumuke kwa dakika kama 30

Unga ukikaribia kuumuka, washa oven joto la 175 ili iwe imepata joto wakati unaweka skonzi kwenye oven. Funua unga kisha upake siagi kwa juu. Oka kwa dakika kama 20 mpaka 25; au mpaka skonzi ziive vizuri

Zikiiva, toa kwenye oven kisha uzipake tena siagi wakati bado za moto. Pakua za moto.

Na kwa wale wenzangu na mie tusio na oven unaweza kutumia jiko la mkaa, unachotak
iwa ni kuweka moto juu na chini kama unapika wali, lakini mkaa wa moto inabidi usiwe mkali sana ni wa kiasi tuu.

Kauli yetu ni ile ile usikurupuke kwa kusoma mara moja na kuenda kutengeneza jaribu kadri uwezavyo ukiona uko sawa basi ndio unatengeneza kwa ajili ya kuuza. Na bei zake huanzia shilingi 100 hadi 500 ni wewe utakavyo amua size yako iweje.

Matumaini yangu umejifunza vyema namna ya kuandaa skozi huu zingatia vyote ili uweze kuandaa vizuri kabisaa nakutakia mafunzo mema. Tukutane ten






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post