Jinsi ya kupika Mahamri

Jinsi ya kupika Mahamri

 

Naam mambo vipi mtu wangu karibu sana kwenye ukurasa wa nipe dili ikiwa tuko ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani basi ni wajibu wangu kuweza kukuelekeza mapishi mbalimbali katika msimu huu.

Leo moja kwa moja tutaelekeza namna ya kupika mahamri ya nazi bila shaka umeshakutana na maandazi haya lakini je wanayaandaa vipi? karibu tujifunze.

Mahitaji

  • Unga wa ngano vikombe 4
  • Sukari kikombe 1/4
  • Tui la nazi zito kikombe 1au 1/2
  • Mafuta uto ya kupikia vijiko vya mezani 2
  • Hamira kijiko cha mezani 1
  • Iliki kijiko cha chai 1
  • Unga wa maziwa vijiko vya mezani 2

Matayarisho

  • Weka unga wa ngano kwenye bakuli uchanganye na unga wa maziwa kisha utengeze shimo katikati.
  • Weka sukari, hamira, iliki, mafuta uto na tui na uzikoroge mpaka sukari iyeyuke
  • Changanya pamoja na unga mpaka uchanganyike vizuri. Hakikisha unga hauwi mgumu na hauwi laini sana kama wa chapatti.
  • Tengeza madonge ya kiasi, uyachovye kwenye unga kisha uyapange kwenye sahani, baraza au sehemu yeyote Safi uliyoimwagia unga na uyafunike. Hakikisha madonge unayapanga mbali mbali ili uyapatie nafasi ya kuumuka/kufuta
  • Yaache madonge Kwa takribani saa zima mpaka yafure yaani (yaumuke) vizuri. Ukitaka yafure haraka utaongeza kipimo cha hamira wakati wa kukanda
  • Bandika mafuta jikoni yaendelee kupata moto
  • Sukuma mahamri na uyakate mara nne ili yawe na shape ya pembe tatu.

Unaweza ukayakata mara mbili yakawa na shape ya mwezi au ukayaacha round. Ila ukitaka mahamri ya round utafanya madonge madogo madogo Sana. Pia usisukume donge Sana mpaka likawa lembamba kama chapati

  • Mafuta yakishika moto vizuri, weka mahamri yako na uyapike mpaka yawe na rangi ya kupendeza pande zote mbili
  • Yatoe kwenye mafuta uyaweke kwenye kitu cha kuruhusu mafuta kupenya
  • Andaa yakiwa moto Kwa mbaazi au chai

Maelekezo

  • Unga wa maziwa unasaidia mahamri kuwa laini zaidi japo si lazima
  • Kama uko sehemu ya baridi hakikisha unaweka hamira ya kutosha na unaweka madonge ya mahamri karibu na moto kwasababu joto ndilo linalosaidia mahamri kuumuka
  • Usiweke sukari nyingi kwasababu inaweza ikasababisha mahamri yasiumuke
  • Hakikisha mafuta yanashika moto vizuri ndio mahamri yafure vizuri yakiwa kwenye mafuta.

Yess mimi nimeishia hapo nawe unaweza ukachanganya na ufundi wako kidogo ukazidi kutoa kitu kizuri zaidi kila la kheri mtu wangu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags