Jinsi ya kupika halfcake kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika halfcake kwa ajili ya biashara

Wengi wetu tunachukulia kupika halfcake ni jambo gumu lakini leo nimekuja kuvunja kauli hiyo kwa kuwaonesha na kuelekezana jinsi ya kutengeneza kitafunwa hicho ambacho wengi wetu hupendelea kukila kwa juice ama chai.

               

MAHITAJI

  • Unga nusu
  • Maziwa/maji
  • Yai 1
  • Sukari vijiko 6 vya kulia
  • Baking powder vijiko 2
  • Zafaran (yellow food coliring)
  • Vanilla powder kijiko 1 au vanilla ya maji (arki)
  • Hiliki 1/2 kijiko
  • Mafuta kwa ajili ya kukaangia
  • Chumvi kidogo
  • Siagi kijiko kimoja

 

JINSI YA KUPIKA

  • Changanya viungo vikavu vyote (unga,sukari,chumvi,hiliki, baking powder)
  • Vunja yai alafu weka katika mchanganyiko wako ...weka siagi changanya vizuri
  • Weka maziwa kisha changanya vizuri hadi utengeze donge moja
  • Kanda hadi iwe laini lakini usiwe laini kama ule wa chapati huu unatakiwa uwe mgumu kidogo kisha subiri kwa dakika 30
  • Katakata halfcakes kutokana na shape unayopenda.
  • Weka karai jikoni kisha acha mafuta yapate moto kidogo na kaanga hadi ziive

ukitaka halfcake zako ziweze kupasuka vizuri inabidi usikaange kama unavyokaanga maandazi hapana cake hizi ukiweka zikaiva basi inabidi ushushe mafuta yapoe ndiyo uweke mkupuo wa pili mpaka utakapo maliza.

Kingine cha kuongezea mwendo ni ule ule lazima ufanye majaribio mara kwa mara kama unahitaji kwa ajili ya biashara hautakiwi kukurupuka siku unajifunza ndiyo siku unayotaka kuwauzia watu, ndugu yangu usifanye hivyo.

 

Kauli yetu ni fanya majaribio mara kwa mara kwa ajili ya kupika kitu bora kwa mlaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags