Jinsi ya kupika chapati  laini za kuchambuka

Jinsi ya kupika chapati laini za kuchambuka

Ooooiiiiiih! yaani mpaka mseme, hivi na nyie mmegundua siku za hivi karibuni biashara hii ya kupika chapati imekuwa katika maeneo mengi yenye mkusanyiko wa watu.

Tena kilichonifurahisha zaidi ni kuona watoto wa kiumbe (vijana) wakiongoza kufanya kazi hiyo, na siyo siri wallah inafaida sana, na ndiyo maana niko hapa kukujuza jinsi ya kutengeneza chapati ili na wewe ujipatie biashara ya kufanya.

Katika pita pita zangu nikauliza baadhi ya wapishi hao wa chapati na kuniambia ni kitafunwa kinachonunuliwa zaidi siku hizi na bei yake huanzia 500-1000.



MAHITAJI

• Unga mweupe wa ngano vikombe 4
• Samli safi vijiko 3 vikubwa
• Chumvii kijiko 1 cha chai
• Maji vuguvugu vikombe 2
• Samli ya kupikia chapati.

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Mimina unga, samli na chumvi kwenye bakuli kubwa then changanya pamoja.
2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
3. Mchanganyiko ukishikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano hivi.
4. Funika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi kwa kuufunika ili hewa isiingie.
5. Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
6. Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
7. Sukuma donge mpaka liwe duara jembamba.
8. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
9. Kunja lile duara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
10. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi
11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
12. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi
13. Pika chapati kwenye frying pan , moto wako uwe wa kiasi.
Mpaka kufikia hapo utakuwa umemaliza pishi lako la kitafunwa hicho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags