Jinsi ya kupamba keki ya birthday (biashara)

Jinsi ya kupamba keki ya birthday (biashara)

Hey guyz mambo zenu, najua wengi wenu mtashangaa kwanini nimekuja na mada hii katika biashara, hivi mnajua mitaani humo nimekuta stori nyingi sana kuhusu watu kujua kupika keki lakini kwenye upambaji ndio hawajui. 

Mie tena mama fukua fukua nikaona isiwe tabu niwaletee watu wangu wa nguvu, na sito tumia muda mrefu kuelekezana kuhusiana na hili, najua watu wengi mnapata tabu mno sasa leo nikaamua niwasaidie ndugu zangu mimi na nyie tena.

Hii ni kwa wale wanaojua kupika keki, kama hujui basi somo la kupika keki linakuja hivi karibuni. Yaani leo tunajuzana mambo mawili kwa wakati mmoja tunaanza kujifunza kutengeneza icing sugar na nyinsi ya kupamba keki yenyewe.

Unasubiri nini ungana nami mwanzo mpaka mwisho…

 

MAHITAJI

  • Vifaa vya kupambia keki
  • Icing sugar
  • Cake ya vanilla au ya radha yoyote uliyokwisha itengeneza tayari

Jinsi ya Kutengeneza Icing sugar

Mahitaji:

  • Sukari ya unga/iliyosagwa vikombe 3
  • Siagi au margarine 1/4 kikombe
  • Maziwa vijiko viwili au vitatu vya chakula(utaongeza kutegemea na uzito wa icing)
  • Vanilla kijiko 1na nusu
  • Food color

Hatua
Chukua bakuli la wastani changanya sukari iliyosagwa, siagi mix na hand mixer yako kwa mwendo mdogo (polepole), kisha ongeza vanilla na maziwa kidogo then malizia kwa kuweka food color. Hakikisha,icing sugar inakuwa nzito kidogo. 

Jinsi ya kupamba keki yako kutumia icing sugar

  • Tumia Spatula kuchota icing sugar na uweke coat ya kwanza kwenye keki.
  • Tumia Cake icer bag, iliyojazwa icing sugar minyia icing kwenye pande zote za keki, zungushia kwa layer tatu na juu.
  • Tumia Icing smoother kusawazisha icing sugar kwenye keki kila kona hadi juu.
  • Kama kuna sehemu zinahitaji icing ya ziada, chukua Spatula chota icing ongezea.
  • Na kama unahitaji kutengeneza maua katika keki yako umia ice piping bag ijaze icing sugar kisha minya icing kwenye kona juu ya keki kuchora maua.

KUANDIKA MANENO KWENYE KEKI
-Tumia icing sugar hiyo hiyo waweza badilisha rangi tu
-Tumia "Toothpick", kuchora dots za maneno unayotaka
-Tumia "Piping bag",kufatisha dots za maneno uliyochora fatisha maneno yote hadi unamaliza.

Na mpaka lufikia hapo utakuwa umeshamaliza kupamba keki yako

Kauli mbiu ni ile ile usikurupuke tuu kuwa leo umepata mteja unaenda kupambia keki my wangu litawakuta jambo, unachotakiwa kufanya ni kurudia rudia mara kwa mara mpaka utakapojiona sasa unaweza kupamba basi ndo utafanya kwa ajili ya biashara, niwaibie tuu siri hakuna biashara inayolipa kama biashara ya keki jaribu utakuja nishukuru badae.

Na kuhusu swala la vifaa nilivyovitaja hapo juu wala visikuchanganye hivi unavipata kwenye maduka makubwa sio yale ya nyumbani kwa mangi hapana, na siku hizi watu wengi wamefungua maduka ya vifaa vya keki hata ukitafta istagram huwezi kukosa utapata kila kitu kinacho hitajika, so kazi ni kwako ni wewe tuu kuchangamkia fursa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags