Jinsi ya kupaka Make-Up

Jinsi ya kupaka Make-Up

Ulimwengu wa fashoon unabebwa na vitu vingi, kutokana na hilo jarida la Mwananchi Scoop, limekusogezea njia za kupaka make-up simple.

Kama inavyofahamika urembo ni kitu muhimu kwa wanawake na kwa sasa imekuwa kawaida mabinti wengi kutumia urembo huo, huku wengine wakitoa pesa kuwalipa make-up artist ili tu waweze kuwapendezesha. Hivyo basi kama unataka kujifunza kupaka make-up pita njia hizi.

Jinsi ya kupaka make-up

Kwanza kabisa itapendeza uso wako uwe safi kisha paka foundation ya rangi yako, baada ya hapo isambaze ikae vizuri usoni

Pili, mara baada ya kumaliza kupaka foundation, kontua zile sehemu ambazo huwa zinatabia ya kutoa mafuta kama vile puani, chini ya macho kwenye paji la uso na kidevuni.

Tatu, paka eye liner machoni kuwa makini usiharibu maana ukipaka vibaya hata make-up yako pia itachekesha

Nne, paka konsila chini ya macho kwenye kidevu paka na kidole ili ku-blend vizuri kisha chukua brush yako bonyeza usisugue ili kufanya iingie kwenye ngozi vizuri hiyo ni ku-highlight

Tano, chukua konsila ya mtu mwenye rangi ya kukuzidi paka kwenye kidevu, kwenye mfupa wa shavu kuanzia kwenye sikio mpaka mwanzo wa jicho, paka kwenye paji la uso, paka kwenye angle ya kichwa.

Sita, sehemu ambazo hutaki zionekane paka konsila ya mtu mweusi, paka ilipoanzia nyusi mpaka kwenye pua hapo unakontua

Saba, paka wanja wako vzuri na eye shadow machoni

Nane, paka lipstick yako vizuri na u-highilight vizuri

Tisa, baada ya hapo paka poda uso wako vizuri kisha kama una spray  ya usoni ni vizuri ukipaka ili make up iweze kudumu. Mpaka hapo utakua umemaliza kupaka make up.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags