Weekend hiyo inanukia kama kawaida ndugu zangu wa urembo na fashion leo bwana time kujua na tatizo ambalo linawaumiza vichwa ndugu ze tu nalo ni Weusi kwenye ngozi ya magoti na kwenye viwiko vya mikono ni jambo linalo wakera wanawake wengi.
Unaweza kun’garisha ngozi ya kwenye magoti na nyuma ya mikono kwa kutumia dawa asilia zifuatazo :
- MAFUTA YA MZEITUNI NA SUKARI.
Chukua vijiko vikubwa vine vya mafuta ya mzeituni kisha changanya na kijiko kikubwa cha sukari kimoja halafu tumia kupaka kama scrub kwenye magoti au nyuma ya mikono kisha tumia kuchua kwa muda wa dakika tatu mpaka tano halafu kaa kwa muda wa dakika thelathini kisha nawa kwa maji ya uvugu vugu. Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku thelathini.
- JUISI YA ALOVERA
Paka fresh juice ya rozera kwenye ngozi ya goti halafu iache kwa muda wa nusu saa kisha tumia kusafisha kwa maji ya moto au vuguvugu.Utafanya hivi kwa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni hadi ngozi yako itakapo anza ku’ngaa.
- BINZARI MANJANO, ASALI NA MAZIWA
Chukua binzari ya manjano kijiko kimoja kikubwa, asali vijiko vine vya chakula na maziwa fresh vijiko vinne vikubwa vya chakula. Vichanganye vyote kwa pamoja kisha tumia kupaka kwenye magoti halafu iachekwa muda wa dakika thelathini kisha naw kwa maji ya uvugu vugu. Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni hadi utakapo pata matokeo utakayo ridhika nayo
- NDIMU
Kata kipande cha ndimu kisha tumia kusugua kwenye magoti. Gotimoja kwa kila kipande. Sugua kwa muda wa dakika tatu hadi tano kisha kaa nayo kwa muda wa lisaa limoja .
Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni hadi utakapopata matokeo utakayo ridhika nayo.
Oooooooooyeeeeeeh nice weekend wapendwa usisahau kudondosha comment yako hapo chini @mwananchiscoop
Leave a Reply