Jinsi ya kuondoa harufu mbaya mdomoni

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya mdomoni

Na Aisha Lungato


Natumai mko powa, Leo kwenye dondoo za urembo tumekuja na suruhisho la tatizo la kutoa harufu kinywani.
Bad breath, sote tunafahamu hili tatizo, sio dogo kama tunavohisi. Na kila mtu ana harufu mbaya mdomoni inategemea tu na usafi wako wa kutunza kinywa chako. Ok kwa wale wenzangu na mimi kutwa mswaki lakini harufu ipo tu shida iko wapi? Fata tips hizi nyepesi ninazokupa baada ya wiki utanipa majibu ikshindikana muone daktari wa meno.


a) SAFISHA ULIMI VIZURI.
Watu wachache sana huchukua zaidi ya nusu dakika kusafisha ulimi, well siri ni kwamba ulimi unatunza sana uchafu katika kinywa, hivyo kuepuka harufu mbaya kama husafishi ulimi vizuri ni historia. Unaweza tumia kijiko kutoa uchafu au nunua tongue cleaner kwa bei nafuu pharmacy. Tuwafundishe watoto tabia hii mapema.


b.) TUMIA MOUTH WASH ZA ASILI NA DUKANI.
Njia nyingine rahisi ya kupata harufu nzuri au fresh breath ni kutumia maji ya chumvi kusuuza mdomo wako. Ni rahisi, haina gharama na haina madhara.Weka chumvi kwa glass ya maji sukutua .Ukiweza kununua mouthwash za dukani kama listerin ni vizuri pia.


c.) MDALASINI NA HILIKI
Hivi viungo vinatumika toka kale na wahenga kuweka harufu nzuri mdomoni.Ukila vyakula vyenye viungo vingi au ukihisi mdomo haueleweki chukua punje ya iriki au kipande cha mdarasini tafuna.Ukiweza chemsha maji ya viungo hivi na sukutua.


d.) APPLE, TANGO NA PERA.
Matunda kama haya yanaongeza mate mdomoni na kuzuia uwepo wa bacteria ambao husababisha harufu mbaya. Kula kipande cha tango au apple hasa baada ya chakula. Pera husaidia wale wanaotoka damu kwenye fizi pia


e.) VINEGAR

Tumia vinegar ya apple inaweza saidia kupunguza uzito pia.Changanya vijiko viwili vya vinegar na glass ya maji halafu kunywa. Au pia waweza sukutua kama mouthwash

.
f.) KUNYWA MAJI MENGI NA GREEN TEA
Ili kuzuia mdomo kukauka hali ambayo husababisha ukuaji wa bacteria mdomoni na husababisha harufu mbaya jitahidi kunywa maji mengi na green tea kila siku.
Hakuna gharama katika njia hizi, vingi ni vitu tunavotumia nyumbani kama viungo na chakula,so why not try today ili kuondokana na hii aibu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags