Jinsi ya kukuza kope halisi

Jinsi ya kukuza kope halisi

Na Aisha Charles

Mambo vipi watu wangu wa nguvu kwa mara nyingine tunakutana tena katika Fashion kupashana habari za urembo na style mbalimbali zinazokiki mjini katika fashion.

Leo katika segment hii tutazungumzia, jinsi gani utaweza kukuza kope zako natural bila kuweka bandia, sasa ni wewe tu kuendelea kusoma ili ujue undani zaidi wa kukuza kope zako halisi.

Kama ilivyo kawaida siku za hivi karibuni wanawake wamekuwa hawapati shida katika urembo wa kope maana hizo bandia zimejaa madukani, kazi ni kwako wewe kununua na kuweka kwa ajili ya urembo.

Ila wamesahau na hawafahamu kuwa kope zao halisi wanaweza kuzikuza na kuwa ndefu kama kope bandia ingawa kuweka kope bandia ni uamuzi wa mtu fulani.

Pia kope bandia ni ukweli usiofichika kuwa zinaweza kuwaonesha watu ni warembo zaidi, haswa kuongeza mvuto wa kimuonekano mbele za watu na ndiyo maana wanawake siku hizi wamekuwa wakishughulika na urembo huo kwa kutaka kope zao ziwe nene na ndefu.

 

Zifuatazo ni mbinu 3 zinazotumiwa sana kukuza kope

  1. usipachike kope bandia juu ya kope zako hali

Unashauriwa ili kuzipa kope zako nafasi ya kukua unatakiwa usiweke kope bandia juu ya kope zako halisi kwa sababu ukiwa na tabia ya kuweka kope bandia kila wakati zinapoteza msingi wa ukuaji wa kope halisia.

Kupachika kope bandia mara kwa mara kunaweza kukuza macho, lakini ukiamua kuivaa kwa muda mrefu huleta madhara ya kukosa kope zaku natural kabisa, pia kunaweza kusababisha kope kulegea kwa sababu ya kuvuta kwa nguvu mara kwa mara wakati wa kuondoa vipodozi katika uso wako.

  1. acha kutumia mascara

Tunajua kabisa kazi ya mascara pia ni kufanya kope zako ziwendefu lakini ni hatari kwa kope zako natural kwa sababu ya kemikali yake.

Hakikisha unaacha mascara, kwa sababu kutokana na matumizi ya kawaida, inaweza kuharibu kwa kiasi kikubwa hali ya nywele na kuwa sababu kuu ya kupoteza nywele.

  1. Acha kusugua macho mara kwa mara

Punguza au acha kabisa  kusugua macho yako sana baada ya kuosha uso wako, unahitaji tu kufuta uso na kitambaa kwa sababau ukifanya hivyo utaondoa uwezo wa kope yako natural kujikaza yenyewe maana kope ni aina ya nywele laini sana sasa unaposugua unasababisha kulegea.

 

Utumiaji wa mask ya ukuzaji wa kope nyumbani

Unaweza ukatumia mask kwa ajili ya kulinda kope zako na kufanya zikue na kuwa nene na hii mask unaweza kuitengeneza ukiwa mwenye nyumbani.

Ikiwa hujui jinsi ya kutengeneza  kwa ukuaji wa kope zako fuata maelekezo hayo japo wengine wanatumia kuweka matango katika macho.

Tafuta mafuta ya castor yaani mafuta ya mnyonyo na majani ya chaji yale ambayo hayajapita matumizi yake

Jinsi ya kupika

Changanya viungo vyote viwili na uhakikishe vimechanganyika ili uweze kupata mask inayofaa kwa ajili ya ukuaji wa kope zako.

Kisha chukua kitambaa cha pamba then weka mchanganyiko wako kwenye kitambaa chako fumba macho na uweke kwenye kope zako na utulie bila kutoa ndani ya dakika 15 baada ya hapo chukua maji ya uvungu osha sehemu ya kope zako fanya hivyo hata mara mbili kwa wiki matokeo yatakuwa mazuri.

Tumia mafuta ya mzeituni na vitamin E

Huu sasa mchanganyiko wake unakuwa na vitu vifuatavyo Almond, Castor, mafuta ya mizeituni matone 5 kila mmoja, vitamini E  matone 5

Jinsi ya kutumia

Weka viungo vyote kwenye chupa halafu changanya viungo kwa kutikisa chupa kwa nguvu kisha paka mchanganyiko huo kila siku kwenye kope za juu na chini hapo hauna haja ya kuosha.

Sababu nyingine za uharibifu afya ya kope

*Matumizi ya  vipodozi usoni ambavyo havina ubora hudhuru ngozi zote za kope na muundo wa nywele, ndiyo sababu kope zako zinakuwa nyembamba na pia hazina afya.

*Ukosefu wa tabia ya kuondoa tongotongo kwenye kope zinakabiliwa zaidi na kuvunjika, ambayo hutokea usiku wakati wa usingizi.

*Kuweka sabuni yenye kemikali nyingi katika kope bila kufahamu madhali wakati una safisha uso.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags