Jinsi ya kukabiliana na wafanyakazi wabishi

Jinsi ya kukabiliana na wafanyakazi wabishi

 

Naam karibu sana kwenye ukurasa wa makala za kazi, ujuzi na maarifa kama ilivyo kawaida yetu hapa ndiyo sehemu sahihi kabisa ya kujifunza masuala kadha wa kadha yanayohusu ajira.

Wiki hii bwana moja kwa moja tutaangazia namna ya kukabiliana na wafanyakazi wabishi katika maeneo ya kazi.

Kama unavyofahamu wafanyakazi wa sampuli hii hawakosekani bwana na mara nyingi mwajiri ukiwa na roho ndogo unaweza kumtimua kabisa kutokana na maudhi yake.

Lakini kabla hujafika hatua hiyo kuna mambo ya msingi ya kufanya ili kuweza kuishi nao licha ya ukaidi wao ,tuanzie hapa sasa kulingana na utawala wa biashara ndogo, wafanyakazi wagumu wanaweza kukasirisha wafanyakazi wenza wengine na mwishowe wanaweza kusababisha hali ya mlipuko ndani ya kampuni yako.

Ikiwa wewe ni meneja au mmiliki, ni wajibu wako kushughulika na mfanyakazi mgomvi kabla hajaathiri tija au upotevu wa wateja. Unahitaji kujua wakati na jinsi ya kukabiliana na mfanyakazi ili kuweka idara yako iendelee vizuri na kuzuia migogoro na wengine.

Twende tukatazame hatua za kufuata ili kukabiliana na sakata hili tuanzie hapa kwanza.

 

Hatua ya 1

Tathmini tatizo linapotokea.

Ikiwa suala liko kwako, sikiliza kwa nini mfanyakazi wako anabishana. Hakikisha kwamba hajisikii kuwa hathaminiwi au ana matatizo na sera ya kampuni au wafanyakazi wengine. Ikiwa tatizo liko kwa mfanyakazi mwenzako, zungumza na pande zote mbili ili kujua kilichotokea. 

Hatua ya 2

Panga mbinu yako.

Hakikisha unapanga mbinu yako ya kukutana na mfanyakazi ana kwa ana badala ya kumkabili mbele ya wengine, hii itakuasaidia kuondosha fedheha ama aibu kwa yule ambaye atabainika kuwa na makosa, si vyema ukamsema mbele ya wafanyakazi wenzake.

Hatua ya 3

Nenda moja kwa moja kwa uhakika na uelezee mfanyakazi kwamba tabia yake inaumiza timu.

Mweleze kwamba anapaswa kufanya kazi kwa bidii zaidi katika kujaribu kufikia malengo ya kampuni. Msaidie kushughulikia masuala yoyote ambayo anaweza kuwa nayo na mfanyakazi mwingine.

Hatua ya 4

Usijibu kupita kiasi kwa hali hiyo.

Uwe mtulivu wakati wote hata kama mfanyakazi anaanza kupaza sauti yake. Ongea kwa uwazi na kwa utulivu ili kupata maoni yako.

Hatua ya 5

Unda mpango wa utekelezaji wa kurekebisha tabia yake ya ubishani.

Hakikisha unafuata taratibu za kinidhamu ikiwa mambo hayatabadilika maana kuna wengine huwa wanakosa nidhamu kabisa, hivyo wawajibishe kulingana na misingi ya kazi.

Hatua ya 6

Fuatilia mfanyakazi ili kuona ikiwa amefanya mabadiliko yoyote katika tabia yake.

Panga mikutano ya ziada kwa muda ufaao ili kufuatilia.

Hatua ya 7

Toa maoni kwa mfanyakazi ambaye anajaribu kudhibiti tabia yake mbaya.

Msifuni kwa kufanya kazi ili kupata suluhisho na hiyo itasaidia kujenga kwa pamoja.

Yap kwa wiki hii ni hayo mfanyakazi mwenzangu na msakatonge, zingatia mbinu hizo utafanikiwa. Tukutane tena wiki ijayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post