Jinsi ya kujitangaza kibiashara kwa bajeti ndogo mtandaoni

Jinsi ya kujitangaza kibiashara kwa bajeti ndogo mtandaoni

Hellow!!! Niaje niaje wafanya biashara ya wajasiriamali ni matumaini yangu mko powa kabisa bwana kama ilivyo ada lazima kila wiki tukutane hapa kujuzana machache kuhusiana na biashara.

Sasa leo tuko hapa tupo na mada ambayo itakusaidia sana na tupo na topic ya namna ya kujitangaza kwa bajeti ndogo mitandaoni. Kama tunavyojua siku hizi asilimia kubwa ya wateja katika biashara wapo mtandaoni.

Na wengi hutumia mitandao ya kijamii kwa njia ambayo haikuzi biashara kupitia mtandao. Na hapa leo tunakujuza vidokezo vya kujitangaza kibiashara kwenye mitandao ya kijamii kwa bajeti ndogo.Na hizi ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kujitangaza…

√ Tumia akaunti za mitandao ya kijamii bure
Unaweza kutumia akaunti yako binafsi kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Twitter, nk. kutangaza biashara yako bila gharama yoyote kwa kuonyesha thamani, elimu na ofa katika huduma/bidhaa yako.

√Tumia ujumbe wa maandishi wa bure
Unaweza kutumia ujumbe wa maandishi mafupi au WhatsApp kuwafikia wateja wako waliopo kwenye orodha yako ya mawasiliano na kuwaeleza kuhusu bidhaa au huduma zako.

√Chapisha picha nzuri na video
Kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram na Facebook, unaweza kuchapisha picha nzuri na video zinazoonyesha bidhaa au huduma zako kwa kuonyesha hatua za mwanzo za kuandaa huduma/bidhaa vilevile unaweza kutumia programu za bure kama Canva au PicMonkey kutengeneza picha nzuri za bidhaa yako.

√Andika maudhui yenye thamani na kuelimisha
Unaweza kuandika maudhui yenye thamani kwa wateja wako kuhusu bidhaa au huduma zako, Maudhui haya yanaweza kuwa katika mfumo wa blogi, vionjo au ushauri.

Tumia mitandao ya kijamii kumiliki soko lako
Unaweza kutumia mitandao ya kijamii ya kibinafsi, kama vile LinkedIn,tovuti(email) kujitangaza kibiashara hii itakusaidia kujenga uaminifu na kuwaleta karibu wateja na kuwaelezea kuhusu biashara yako.

Tumia matangazo katika kurasa za kijamii
Matangazo katika kurasa za mitandao ya kijamii yanaweza kuwa na gharama kidogo na yanakupa nafasi ya kufikia idadi kubwa ya watu kwenye mitandao hiyo mitandao ni ile ile tuu kama vile Facebook Ads au Instagram Ads ili kuwafikia wateja wako kwa urahisi.Kwa kuzingatia njia hizi, unaweza kujitangaza kibiashara kwenye mitandao ya kijamii kwa bajeti ndogo au hata bila gharama yoyote katika kukuza biashara yako.

Siku zote biashara inataka uvumilivu na biashara nyingi za siku hizi bila kuzitangaza haziwezi kufanikiwa so chakufanya kikubwa kabdri uwezavyo kupitia mitandao ya kijamii ulionayo ifanye kuwa fursa ya wewe kupata wateja. Usitumie mitandao yako ya kijamii kwa kujipost wewe mwenyewe wakati unabiashara.

Haya sasa watu wangu wa nguvu wafanyabiashara na wajasiriamali usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop ili uweze kujifunza kutokana na mada mbali mbali za kuelimisha na kuburudisha.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post