Jinsi ya kuficha baadhi ya SMS za Whatsapp

Jinsi ya kuficha baadhi ya SMS za Whatsapp

Je unatamani kuficha baadhi ya chats zako wengine wasizione? Kama ulikuwa unatumia njia ya kufungua WhatsApp yako na kuingia kwa Face ID au Passcode, sasa unaweza kuachana na mchezo huo na badala yake ukafisha SMS chache tu unazotaka zisisomwe na wengine.

Kwa watumiaji wa simu za Iphone fungua WhatsApp katika uwanja wako wa meseji tafuta jina la mtu unayetaka kuficha SMS zake.

Kwa mtumiaji wa Iphone hakikisha unatafuta jina kwa kupandisha juu au kushusha chini chats na siyo kwa ku-search jina kwani ukifanya hivyo hautaletewa machaguo.

Mara baada ya kuzifikia SMS za mtu unayetaka ku-lock usifungue kuingia kwenye chats zenu badala yake bonyeza kwa nguvu kwenye jina kama unavyofanya ukitaka kusoma SMS za mtu bila kuzifungua.

Baada ya hapo utaletewa machaguo unachotakiwa ni kubongeza Lock Chat mara baada ya kufanya hivyo, utatakiwa kuchagua njia ya kuzifungia inaweza kuwa Face Id au Pass code.

Chagua njia unayotaka baada ya hapo jambo lako litakuwa limekamilika hakuna mtu atayeweza kusoma SMS hizo.

Ukitaka kufika kwenye SMS ulizozifungua unaingia kwenye uwanja wako wa WhatsApp kisha una-scroll sms kwenda chini utaona kitu kama kufuli bonyeza uingie kwenye SMS ulizoficha.

Itaendelea wiki ijayo kwa watumiaji wa simu za Android.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post