Jinsi ya ku-post video,picha bila kupoteza ubora

Jinsi ya ku-post video,picha bila kupoteza ubora

Instagram ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu na wenye watumiaji wengi zaidi duniani

siku za nyuma ilikuwa ukirudia kupandisha (ku-post) video mara kadhaa inapoteza ubora. hivyo kutokana na mapenzi mema ya wamiliki wa mtandao huu wamekuja na njia mpya itakayowawezesha watumiaji ku-post video au picha na zikabaki na ubora wake uleule.

Cha kufanya ili video, picha yako isipunguze ubora ingia kwenye ukurasa wako wa Instagram na kisha nenda hadi kwenye eneo lenye vidoti vitatu juu upande wa kulia bonyeza, ingia eneo lililoandikwa settings and privacy.

Shuka chini hadi eneo lililoandikwa Data usage and media quality kisha kubali kuruhusu kuingia eneo lililoandikwa upload at highest quality

Ukifika hapo hata uki-post faili kubwa litafika kama lilivyo usiogope ukiona linachukua muda mrefu kuwa na subira litafika likiwa na ubora uleule






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags