Jina la mtoto wa Rihanna lazua gumzo

Jina la mtoto wa Rihanna lazua gumzo

Baada ya watu kusubiri kwa muda mrefu kujua jina la mtoto wa pili wa Rapper kutoka nchini Marekani Asap na mpenzi wake Rihanna hatimaye jina la mtoto huyo limewekwa wazi ambapo wamempa jina la Riot.

Jina hilo limezua gumzo kwa sababu linamaanisha fujo au ghasia ambapo mtoto huyo alizaliwa Agosti 1 mwaka huu katika hospitali ya Cedar Sinai Los Angeles nchini Marekani, jina lake kamili likiwa ni Riot Rose Mayers.

Ikumbukwe kuwa Rapper huyo mwanzoni mwa mwaka huu aliachia wimbo aliyomshirikisha Pharrell Williams ulioitwa ‘Riot’ ambapo baadhi ya mashabiki waliamini kuwa wimbo huo huenda ukawa ndiyo chanzo cha jina la mtoto huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags