Jifunze  simu janja zinavyo tengenezwa

Jifunze simu janja zinavyo tengenezwa

Mambo niaje! msomaji wa Mwananchi Scoop? Leo kwenye kipengele cha Smartphone bwana nakuletea namna simu janja zinavyotengenezwa bwana au sio fuatilia dondoo hii ili uweze kujifunza zaidi.

Simu janja ni kifaa cha kielektroniki kinachowezesha mawasiliano na chenye uwezo wa kuchakata taarifa  mithili ya kompyuta.

Kutokana na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kama kupiga picha, kuingia mtandaoni na kupakua programu mbalimbali zinazorahisisha kazi simu janja zimekuwa na umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku.

Kuna makampuni mengi yanayohusika na kutengeneza simu janja, kubwa zikiwa ni Apple na Samsung na zingine ni OPPO, Vivo, Huawei, Xiaomi na Tekno. Nchi ya China ndo inayoongoza kwa utengenezaji wa simu ikifuatiwa na nchi ya India. Simu janja zimekuwa zikitengenezwa kwa wingi na mara kwa mara kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia.

Hatua ya kwanza katika utengenezaji wa Simu janja huwa ni utengenezaji wa sampuli ambayo hutumika kama mwongozo wa kutengeneza simu janja zingine nyingi. Sampuli hiyo inakuwa na vielelezo vyote vya muhimu kama uzito wa simu, ukubwa wa simu, kioo na kamera, matundu ya spika na chaja. 

Utengenezaji unapoanza fremu ya nje ndo huwa ya kwanza kutengenezwa ambayo hupitia katika hatua mbalimbali ikiwemo kutoboa matundu ya misumari, kukata eneo la kuweka antena, kung’arisha na kukomaza fremu kwa kuipasha moto.

Wakati huo vioo vya simu janja huwa vinaandaliwa hapo hapo kiwandani au huwa vinatolewa kiwanda kingine na kupitia vipimo mbalimbali vya ubora ili kuhakikisha kuwa bidhaa kamili haina hitilafu zozote zile za kiufundi kabla ya kumfikia mteja.

Baada ya hapo wafanyakazi mbalimbali wa kiwandani huhusika na kuunganisha vifaa vyote vya ndani vinavyounda simu janja kama spika, kamera, kioo, fremu, betri, sakiti bodi na antena. Wafanyakazi hawa hutumia umakini wa hali ya juu katika uwekaji wa vifaa hivi ili kulinda ubora wa bidhaa.

Hatua ya mwisho katika utengenezaji huwa ni upimaji wa ubora wa bidhaa ambapo timu ya wafanyakazi mbalimbali wa kiwandani watahusika na kupima kitu kimoja kimoja katika kila simu kabla ya kupakiwa na kwenda kwa mteja.

Upimaji huu huhusisha pia na uwezo wa simu kuvumilia misukosuko kama kuangushwa sana, kuchomekwa na kuchomolewa chaja mara kwa mara, kioo kusuguliwa kwenye nguo mara kwa mara na simu kunyeshewa na mvua kidogo au kuwa katika mazingira yenye unyevunyevu. 

Simu zinazokidhi vigezo vyote na kufaulu vipimo vyote vya ubora hupakiwa na kusafirishwa sehemu mbalimbali duniani na kuanza kutumika na wateja. 

Ebwana eeeh!!!!! Hivyo ndivyo mambo yanavyokuwa katika kufanikisha kutengeneza simu janja this is Smartphone bwana enjoy!!!!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post