Jerry Silaa: Le Mutuz hakuwa mnafki

Jerry Silaa: Le Mutuz hakuwa mnafki

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa amesema William John Malecelea maarufu kama Le mutuz enzi ya uhai wake alikuwa ni mtu aliyependa kusema ukweli nyakati zote na hakuwa mtu wa kumung'unya maneno.

Silaa ameyaeleza hayo katika ibada ya kuaga na kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Le mutuz, ibada ambayo imefanyika leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

“Enzi ya uhai wake Le mutuz miongoni mwa Sifa zake hakuwa mtu wa kupindisha Ukweli, hakuwa mnafiki kwenye ukweli atasema ukweli” amesema Silaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags