Jennifer Lopez na Ben wauza nyumba, Wadaiwa kuachana

Jennifer Lopez na Ben wauza nyumba, Wadaiwa kuachana

Mwanamuziki wa Marekani Jennifer Lopez na mumewe Ben Affleck wanadaiwa kuachana baada ya kuuza nyumba yao waliyoijenga pamoja kwa dola 60 milioni.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ News inaelezwa kuwa wawili hao wameuza nyumba hiyo waliyoijenga mwaka jana huku kukiwa na tetesi kuwa ndoa yao haipo tena ingawa hakuna aliyewasilisha ombi la talaka.

Hata hivyo pamoja na kuuza nyumba yao imeripotiwa kuwa gharama ya uuzaji wa mjengo huo ni tofauti na gharama waliyoitumia kujenga na kuboresha ambapo kwa sasa Ben anadaiwa kupanga nyumba mpya huku ikiwa haijafahamika sehemu ambayo Jennifer anayoishi.

Wawili hao walionekana kutokuwa pamoja tangu Februari baada ya kutoka filamu ya ‘This is Me’ iliyo zungumzia uhalisia wa mahusiano yao na hali halisi ya utengenezaji wa album ya Lopez.

Lopez na Ben walianza mahusiano yao ya uchumba mwaka 2021 na kufunga ndoa mwaka 2022.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post