Jela yamuita tena Chris Brown

Jela yamuita tena Chris Brown

Muimbaji maarufu kutoka nchini Marekani Chris Brown ameibua msala mpya ambao unaweza kumletea hatari kubwa ya kumpeleka jela, kwani ameripotiwa kwamba endapo atarudi tena Uingereza basi anaweza kuishia gerezani kufuatia tukio la uhalifu alilolifanya.

Mapema mwezi feb mwaka huu 2023 wakati Chris Brown akiwa kwenye ziara yake ya "under the influence" alishtakiwa kwa kumpiga na chupa mtayarishaji mmoja wa muziki wakiwa club huko mjini London, nchini Uingereza.

Chanzo kimoja kimeiambia "The sun"; Brown anafahamu fika kabisa akirudi Uingereza atakamatwa, na hivyo anafanya kila aliwezalo kukwepa msala huo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post