Jela miaka 35 kwa kuiba na kuuza viungo vya maiti

Jela miaka 35 kwa kuiba na kuuza viungo vya maiti

Mmiliki wa chumba cha kuhifadhia maiti na mama yake wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 35 jela baada ya kupasua mamia ya miili na kuuza sehemu za miili bila ridhaa ya familia za wateja wao.

Waendesha mashtaka wanasema Megan Hess, 46, na mama yake Shirly Koch, 69, walikatakata maiti 560 na kuuza viungo vya miili bila idhini kati ya mwaka 2010 na 2018. Hess atafungwa jela 20, huku Koch akihukumiwa miaka 15 jela.

Na hii imebainika baada ya ndugu kadhaa ambao walikuwa wamemtumia Hess kuchoma maiti za ndugu zao baadaye waligundua kuwa walikuwa wamepokea majivu yaliyochanganywa na mabaki ya watu wengine.

Kulingana na waendesha mashtaka huko Colorado, wawili hao mama na binti walikata sehemu za miili, na wakati mwingine miili mizima kuiuza.

Hess ambaye anaendesha biashara ya Jumba la Mazishi la Sunset Mesa katika mji wa Montrose  alitoza familia hadi $1,000 kwa uchomaji maiti ambao haukufanyika na badala yake kuikabidhi miili hiyo kama michango bila malipo.

Mmmmmmmmh! Jamani jamani hivi Dunia inaenda wapi maani siku hizi watu hawaogopi wala hawana huruma kabisa. dondosha komenti yako hapo chini na utueleze ni hukumu gani ungefaa kwa mama na mwanae?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags