Je kukataza suruali za kubana, Vimini, na Milegezo ni njia ya kuboresha maadili

Je kukataza suruali za kubana, Vimini, na Milegezo ni njia ya kuboresha maadili

Kufuatia taarifa ya jana iliyo ripotiwa na mwananchi kuhusiana na sheria iliyowekwa Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha ikihusisha kuimarisha maadili kwa kukataa baadhi ya mambo kwa vijana.

Ikiwemo kupigwa faini ya sh 50000 kwa msichana yeyote atakayevaa suruali za kubana au sketi fupi 'vimini', na kwa kijana wa kiume kusuka nywele au kunyoa pembezoni mwa kichwa na kuacha nywele katikati 'kiduku', kuvaa hereni au kuvaa suruali inayoonyesha makalio.

Tuambie nini mtazamo wako, je mambo waliyokataza yanaweza kuimarisha maadili au iangaliwe njia nyingine ya kufanya ili kuwa na vijana wenye nidhamu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post