JB atoa sababu za kurudia wahusika kwenye filamu

JB atoa sababu za kurudia wahusika kwenye filamu

Licha ya kuwa nchini wameendelea kuibuka waigizaji wengi chipukizi, lakini baadhi ya waandaaji wa filamu wanaonekana kurudia wasanii katika kazi zao, jambo ambalo limekuwa likizua mijadala kwa wadau wa filamu huku wengine wakionesha kiu yao ya kutaka kuona vipaji vipya sokoni.

Akizungumzia tabia ya kurudia wasanii, mwigizaji na mwongozaji filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', amesema sababu za wazalishaji filamu kufanya hivyo ni uwepo wa waigizaji wachache wenye uwezo.

JB amesema anatamani wapate waigizaji wapya wenye uwezo mkubwa zaidi, ndiyo maana yuko bize kufanya usaili wa waigizaji wapya ili kuleta sura mpya kwenye uigizaji kwani mashabiki wamechoka kuona waigizaji wale wale wasiobadilika.

"Mashabiki wasitulaumu sana kwa wazalishaji kurudia wasanii wale wale kwenye filamu na tamthilia. Sababu ni tasnia ya uigizaji ina waigizaji wachache wenye uwezo wa kuigiza. Ndiyo sababu mashabiki wanaona hawabadiliki.

"Binafsi nimeligundua hilo na natamani nipate waigizaji wapya wenye uwezo mkubwa zaidi, ndiyo maana niko bize sasa hivi kufanya usaili wa waigizi wapya ili kuleta sura mpya kwenye uigizaji. Ukiingia kwenye ukurasa wangu wa Instagram, utaona usaili unavyoendelea. Yaani nimedhamiria na najua watapatikana tu," amesema JB.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags