Jay Z atuhumiwa kubaka akiwa na Diddy

Jay Z atuhumiwa kubaka akiwa na Diddy

Mwanamuziki wa Marekani Jay-Z anatuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13 tukio ambalo linadaiwa kufanyika akiwa na Diddy.

Kwa mujibu wa NBC News kwenye taarifa yao wamesema mshtakiwa huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37 anasema tukio hilo lilitokea mwaka 2000 baada ya sherehe za ugawaji wa Tuzo za Videos za MTV.

Kesi hiyo ambayo iliwasilishwa hapo awali mnamo Oktoba,2024 maeneo ya Kusini mwa New York huku wakimtaja Combs Diddy kama mshtakiwa wa kwanza, imewasilishwa tena Jumapili ya Desemba 8, 2024 huku Jay Z akitajwa kuwa miongoni mwa watuhumiwa.

Hata hivyo, masaa machache Jay-Z ametoa kauli juu ya shitaka hilo akisema amesikitishwa na mwanasheria ambaye amefungua shtaka hilo bila kupepesa macho akiliita shtaka hilo ni upuuzi na lina lengo la kumkamua pesa na kumdhalilisha.

Aidha kwenye andiko lake pia ameiomba radhi familia yake akiwemo mkewe pamoja na watoto wake kwa kilichotokea ambapo kimechafua taswira yake.

“Umefanya kosa kubwa sana kufikiri na kuamua kwamba watu mashuhuri wote tupo sawa. Mimi sipo kwenye dunia yako. Mimi ni kijana mdogo ambaye nimetoboa toka Brooklyn.

“Huwa hatuchezi hii michezo, tuna heshima zetu. Tunawalinda watoto, unaonekana unataka kuwaonea watu kwa ajili ya faida zako binafsi. Ni watu wako pekee wenye kufikiri sawa na wewe ndio wanaweza kuamini madai haya kipuuzi dhidi yangu.” Jay-Z ameandika kupitia tamko lililotolewa na Roc Nation.

Baada ya kanusho hilo wakili wa mwanamke aliyemshitaki Jay Z, Tony Buzbee amedai msanii huyo alijaribu kuwanyamazisha wateja wake na kumtisha.

“Mteja wangu hakuhitaji hata sarafu, Jay Z sio tu amenishitaki bali pia amenishambulia pamoja na kunitishia, tutaacha mashitaka yaongee yenyewe na tutaweka ukweli wote mahakamani,” - Tony ameeleza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags