Jay Melody ajipata Boom Play

Jay Melody ajipata Boom Play

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Jay Melody amefikisha zaidi ya streams milioni 300 kupitia mtandao wa kuuzia muziki Boom Play Music, akiwa na zaidi ya nyimbo 40 kwenye akaunti yake.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtandao huo wamechapisha taarifa inayoeleza kuwa Jay Melody amefikisha streams milioni 300 mwaka huu.

“Mwaka jana, tarehe kama ya leo, tulimpongeza @realjaymelody na streams 200M. Leo hii ndani ya mwaka 2024, tunampongeza tena kwa kufikisha streams zaidi ya milioni 300 kwenye app ya #Boomplay”



Kupitia mtandao huo wimbo unaoongoza kwa streams katika akaunti ya Jay ni ‘Nakupenda’ wenye zaidi ya streams milioni 82, huku mpaka kufikia sasa unazaidi ya wasikilizaji milioni 33 kupitia mtandao wa YouTube.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa msanii huyo ameingia katika kinyanganyiro cha kuisaka Tuzo ya TMA Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka kupitia wimbo 'Nitasema'






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags