Jason Derulo anaamini Diddy hana hatia

Jason Derulo anaamini Diddy hana hatia

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jason Derulo amkingia kifua mkali wa Hip-hop Diddy kwa kudai kuwa mwanamuziki huyo hana hatia.

Derulo ameyasema hayo wakati alipokuwa akipiga picha na mashabiki katika mitaa ya New York ambapo alieleza kuwa anaamini Diddy hana hatia mpaka pale itakapothibitika kuwa na hatia.

Ingawa maoni ya Jason yalikuwa mafupi, uamuzi wake wa kumuunga mkono Diddy hadharani ni muhimu, haswa katika tasnia ya muziki ambayo wengi wamechagua kukaa kimya juu ya suala hilo.

Hata hivyo mpaka kufikia sasa Diddy bado hajakamatwa wala kushitakiwa kwa uhalifu lakini uchunguzi dhidi ya mashitaka yanayomkabili bado unafanyiwa kazi na Serikali nchini humo.

Iklumbukwe kuwa Diddy na Derula waliwahi kufanya kazi pamoja ambapo Jason alikuwa akiwaandikia nyimbo Combs pamoja na wasanii wake mwaka 2000.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags