Jason Derulo aendelea kuitangaza Komasava

Jason Derulo aendelea kuitangaza Komasava

Wakati akiwa kwenye ziara yake ya ‘Nu King’ iliyofanyika nchini Ujerumani, mwanamuziki Jason Derulo ameendelea kuutangaza wimbo wa ‘Komasava’ kwa kuutumbuiza katika show yake hiyo.

Utakumbuka kuwa Derulo alitumbuiza wimbo huo pia Agosti 10 katika show yake iliyofanyika ‘Selman Stërmasi Stadium’ nchini Albania na Kroatia huku akiripotiwa kuutangaza wimbo huo katika ziara yake inayo kadiriwa kutamatika Novemba mwaka huu.

‘Komasava Remix’ ni wimbo wa #Diamond aliyowashirikisha wasanii kama Jason Derulo, #KhalilHarisson na #Chley ambapo video yake mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji milioni 11 kupitia mtandao wa YouTube ikiwa na wiki tatu tu tangu kuachiwa kwake.

Aidha wimbo huo unazidi kukonga nyoyo za watu wengi kutokana na kuwepo na lugha tofauti tofauti duniani ikiwemo Kifaransa, Kichina, Kihindi na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags