Jake Paul na Mike Tyson watazichapa Novemba 15

Jake Paul na Mike Tyson watazichapa Novemba 15

Baada ya pambano la mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Marekani Mike Tyson na Jake Paul kughairishwa kufuatia na tatizo la kiafya alilokuwa nalo Tyson, sasa imepangwa tarehe mpya ya wawili hao kupanda.

Tarehe mpya iliyotajwa ni Novemba 15, 2024 kwenye Uwanja wa AT&T huko Arlington, Texas.

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika Julai 20 katika uwanja huo huo pamoja na kuoneshwa moja kwa moja (live) katika mtandao wa Netflix.

Mei 27 mwaka huu Tyson alipata dharura ya kiafya ndani ya ndege na kupatiwa matibabu humo humo akiwa anatoka Miami kuelekea Los Angeles lakini siku mbili baadaye aliweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa yupo fiti asilimia 100.

Aidha siku chache baadaye uongozi wa pambano hilo ulitoa taarifa ya kughairisha mpaka pale tarehe mpya itakapo pangwa baada ya hali ya Tyson kuwa mbaya.

Mara ya mwisho kwa Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu kuingia ulingoni ilikuwa ni mwaka 2020, ambapo lilikuwa ni pambano la raundi nane dhidi ya Roy Jones Jr huko Los Angeles.

Aidha kwa upande wa Jake Paul amekuwa na mafanikio kadhaa katika mchezo huo katika rekodi yake ameshawahi kuwashinda nyota wa zamani wa UFC kama Nate Diaz, Anderson Silva, Tyron Woodley, Andre August na Bourland.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post