Jada Smith: Nywele zimeanza kuota

Jada Smith: Nywele zimeanza kuota

Muigizaji na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani Jada Pinkett Smith ameonyesha muonekano wake mpya huku akieleza kuwa nywele zake zinarudi.

Jada Pinkett Smith alionekana kuwashangaza wengi alipo onesha nywele zake mpya za mvi huku akikiri kuwa nywele zake zinazidi kukua licha ya kuwa na alopecia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram muigizaji huyo ali-share picha yake ya kwanza ikimuonesha akiwa hana nywele (kipara) na picha ya pili ikionesha kuwa nywele zake zimeota.

Ikumbukwe tu Jada amekuwa akikabiliana na ugonjwa wa alopecia kwa miaka mingi na alitangaza ugonjwa wake kwa mara ya kwanza kwenye kipindi chake cha Red Table Talk, mwaka wa 2018.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags