Jada Smith alichumbiwa na Tupac

Jada Smith alichumbiwa na Tupac

Jada Pinkett Smith anaendelea kushika vichwa vya habari kutokana na mahojiano anayofanya akielezea maisha yake na kilichomo kwenye kitabu chake kipya, awamu hii akiwa kwenye mahojiano na podcast ya ‘All the Smoke’ ya Showtime ameeleza kuwa alichumbiwa na Tupac Shakur.

Inafahamika kuwa wawili hao enzi za ujana wao walikuwa na ukaribu, na ndivyo Jada ameedelea kuongelea urafiki wake na Tupac na kudai kuwa kipindi Tupac yupo gerezani Rikers, alipoenda kumtembelea msanii huyo alimchumbia na kuomba amuoe.

Jada amedai kuwa alikataa japo alielewa kuwa kwa kipindi hiyo msanii huyo alihitaji mtu ambaye ageweza kufanya naye maisha lakini alikataa na kumueleza Tupac kuwa hakuna ulazima wa wao kuoana.

Ikumbukwe kuwa Tupac hadi anafariki dunia mwaka 1996, alikuwa tayari na mchumba mwingine aitwaye Kidada Jones






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags