Jada na Smith walitengeneza chumba cha siri

Jada na Smith walitengeneza chumba cha siri

Licha ya Will Smith na Jada kutengana kwa miaka 7 sasa lakini waliutumia vizuri muda wao wakati watoto wao walipokuwa wadogo.

Jada kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ameweka wazi kuwa kipindi watoto wao walipokuwa wadogo yeye na Smith walitumia muda mwingi kuwa karibu na hii inawezekana kuwa sababu ya wawili hao kutopeana talaka.

Mwanadada huyo ameweka wazi kuwa walilala na watoto wao hadi walipofika umri wa miaka kadhaa ambapo Jada aligundua kuwa Smith amechoshwa kulala na watoto ndipo Jada akaamua kutengeneza chumba cha siri lakini baada ya muda watoto hao waligundua chumba hicho.

Ikumbukwe tu Jada wiki iliyopita kufutaia mahojiano yake aliweka wazi kuwa walitengana kwa siri miaka 7 japo wawili hao hawana mpango wa kupena talaka.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags