Iphone zitakuwa na uwezo kwa kurekodi mazungumzo

Iphone zitakuwa na uwezo kwa kurekodi mazungumzo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya simu za Iphone imeweka wazi kuwa katika mfumo wao wa ‘iOS 18.1’ wanatarajia kufanya maboresho katika upande wa kupiga simu ambapo wanatarajia kuweka mfumo wa kurekodi mazungumzo.

Call Recording itawawezesha watumiaji wa iPhone kurekodi mazungumzo ya sauti na kuhifadhi sauti kwenye app ya Notes, mbali na hilo pia itaandika mazungumzo ambayo umeyazungumza kwa mfumo wa maandishi.

Licha ya kuweka mfumo huo ambao utawawasaidia wengi, jambo ambalo watumiaji wanatakiwa kuwa nalo makini na kulizingatia ni kuwa utakapo bonyeza kitufe cha kurekodi mazungumzo basi kunamlio utatoka kwa ajili ya kumjulisha mtu unayezungumza naye kuwa unarekodi mazungumzo hayo.

Mfumo huo wa kurekodi mazungumzo hautatumia Apple Intelligence (AI) kufanya kazi, utaweza kutumia bila internet na ili kupata summary ya mazungumzo ndio itakulazimu kutumia Apple Intelligence.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags