Bunge la Indonesia leo Jumanne limeidhinisha sheria mpya ya uhalifu ambayo itafanya kushiriki ngono nje ya ndoa kuadhibiwa kwa mwaka mmoja jela.
Sheria hiyo ambayo itatumika kwa Waindonesia na wageni inajumuisha sheria kadhaa za "maadili" na inafanya kuwa kinyume cha sheria kwa wanandoa ambao hawajaoana kuishi pamoja na kufanya ngono.
Mpenzi wa mtu au wazazi wanaweza kuwaripoti kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa. Uzinzi pia utakuwa ni kosa ambalo watu wanaweza kufungwa jela.
Baadhi ya maeneo ya Indonesia tayari yana sheria kali za kidini kuhusu ngono na mahusiano kabla ya ndoa.
Jimbo la Aceh linatekeleza sheria kali za Kiislamu na limewaadhibu watu kwa kucheza kamari, kunywa pombe na kukutana na watu wa jinsia tofauti. Sheria hizo mpya za uhalifu hazitaanza kutumika hadi baada ya miaka mitatu.
Hahahhahah! Make hapa kwanza ncheke hivi ni vipi kama sheria hii ikipitishwa nchini kwako? Imagine itakuwaje embu dondosha komenti yako hapo chini.
Chanzo BBC
Leave a Reply