Imethibitika wanawake wenye maumbo mparaganyiko huharibu mambo kwa kujistukia

Imethibitika Wanawake Wenye Maumbo Mparaganyiko Huharibu Mambo Kwa Kujistukia

Katika utafiti uliochapishwa hivi karibuni katika jarida la Personality and Social Psychology imethibitika kwamba wale wanawake wenye maumbo mparaganyiko yaani yasiyovutia huwa hawaridhiki na  mahusiano yao na wenzi wao kwa kujistukia kwamba hawana mvuto kwa wapenzi wao.

Hali hiyo inachangiwa zaidi na kutokujiamini kwa kujiona kama hawana hadhi ya kuwa na hao wapenzi walio nao kutokana na ile hali ya kujiona hawana maumbo yenye kuvutia kama wanawake wengine.

Katika utafiti huo uliofanywa na mtaalamu wa saikolojia Allanah Hockey na timu yake, walibainisha kwamba dhana hii ya wanawake wenye maumbo yasiyovutia kujistukia inaweza ikaelezewa kitaalamu kama “projection bias.”

Yaani ile hali ya kuamini kwamba kile unachowaza ndicho wengine wanachowaza.

Wataalamu hao walifanya utafiti wao kwa wanandoa 197 ambao wameishi kwenye ndoa kwa miaka miwili na ushee. Wanandoa wote walijibu maswali waliyopewa katika utafiti huo kuhusiana na kuridhika na maumbo ya wenza wao katika mapenzi. 

Pia waligusia kuhusu kuvutia kwa maumbo ya wapenzi wao kama wanaridhika na maumbo yao na mwisho walitoa maoni yao kama wanadhani wangependa wapenzi wao wawe na maumbo ya namna gani yanayovutia au wanayoyatamani.

Katika kupitia majibu ya maswali hayo wataalamu hao waligundua kwamba jinsi wanaume na wanawake wanavyojiona wanavutia kimaumbo na kimuonekano na ndivyo ile hisia ya kujistukia kwamba hawana mvuto inakuwa ndogo.

Lakini kwa upande wale wenye maumbo mparaganyiko yasiyovutia hususan wanawake ndiyo walioibuka kidedea kwa kujistukia kwamba hawana mvuto kwa waume zao tofauti na wanaume.

Hata hivyo kama unadhani unaweza kubadili hali hiyo kwa kufanya mazoezi basi fanya lakini kama umbo ulilo nalo ni personal na huwezi kulibadili basi jiamini na usimame kwenye ndoa yako bila kujali maoni ya watu. 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post