Ikibidi Harmonize ashushe pini kila wiki

Ikibidi Harmonize ashushe pini kila wiki

Hii nimeisikia kwa watu kadhaa kitaani. Kwamba Konde anatoa 'traki' mfululizo. Eti hii inaweza kufanya akachokwa fasta kama ilivyotokea kwa Aslay. Tukiacha hizi hisia ziendelee katika vichwa vya wachache siyo sawa. Wacha tusemane kidogo tu, ili kuwekana sawa.

Kwanza kwa lyrics, melody na content hakunaga kama Konde Boy. Huyu mchizi ni namba moja kwa sasa hata ukikataa. Kumkataza asitoe ngoma mfululilizo ni kumkataza asifanye kazi. Mbona radio, magazeti na runinga vipo hewani 'deile' na hatuchoki kutazama, kusikiliza na kusoma?

Kama ana content, sauti, melody na lyrics kali kwanini asitoe ngoma kila wakati? Kumbuka muziki ni kama soka, ukiwa kwenye kilele cha mzuka ni kupiga back to back utakavyo. Hivi sasa mwezi mzima ukiwa kimya mwezi tu unapotea jumla, kuna wasanii wengi sana.

Na pesa ya muziki ipo kwenye platforms siyo album wala shows. Asipotoa mara kwa mara unataka apate wapi pesa? Kama akili yake inafanya kazi acha atoe ngoma back to back maana uwezo huo anao. Hata kitaa wananchi wanahitaji kumsikiliza kila wakati, ikibidi ashushe pini kila wiki.

Wabongo bana! Kiba wanamlalamikia hatoi ngoma mara kwa mara. Konde Boy wanamlalamikia kwa kutoa mara kwa mara. Kama msanii ana akili na uwezo ni haki yake kutoa kazi kila wakati kwani muziki ni maisha ya kila siku. Diamond katoa ngoma ngapi mwaka huu tu? Jibu kaa nalo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post